KFS Tanzania imetangaza rasmi leo kuwa ndio kituo pekee nchini kitakachorusha matangazo ya michuano ya Kombe la Dunia 2018 (FiFA World Cup 2018) bure inayotarajiwa kuanza tarehe 14 Juni 2018 na kumalizika tarehe 15 Julai 2018 nchini Urusi.
KFS Tanzania wakishirikiana na kituo cha Televisheni cha TBC watarusha matangazo hayo moja kwa moja.
Kutakuwa na mechi 32 zikiwemo zote zitakazochezwa na timu za Afrika, Robo Fainali, Nusu Fainali pamoja na Mechi za mwisho ya Fainali,hii si ya kuikosa hata kidogo.
KFS inapatikana kupitia King'amuzi cha Startimes Chanel 103, Continental Chanel namba 07 na Ting Chanel namba 36
Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt. Ayub Rioba(Kulia) akisaini Mkataba wa makubaliano kati ya KWESE free Sports (TV1) na TBC kuonesha Kombe la Dunia kuanzia Juni 14,2018