Meneja
Mawasiliano wa Shirika la Hifadi za Taifa ,(TANAPA) Pascal Shelutete
akizungumza mara baada ya wageni hao kushuka baada ya kufanikiwa kufika
kilele cha uHuru kwa kutumia Baiskeli.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
SHIRIKA
la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limesema litafikiria matumizi ya Boda boda
na Bajaji kwa wageni watakao hitaji kutembelea Hifadhi zake endapo
yatajitokeza maombi ya kutosha kuhusu matumizi ya vyombo hivyo.
Hatua
hiyo inatokana na bidhaa mpya ya Utalii wa kutumia Baiskeli
iliyoanzishwa hivi karibuni katika Hifadhi za Taifa za Mlima Kilimanjaro
na Arusha kuanza kuwa kivutio kwa watalii kutoka nchi mbalimbali
walioanza kufanya utalii wa Baiskeli.
Miongoni mwa watali hao ni pamoja na mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli ,Juanito Oiarzabal
aliyeweka rekodi ya kuwa Mhispania wa kwanza kupanda Mlima Kilimanjaro
huku akitumia saa 31 akiendesha baiskeli katika siku tano hadi kufika
kilele cha Uhuru.
Juanito na wenzake wawili , Eduardo
Pascuaz na Ramon Abecia waliianza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro
kwa kutumia Baiskeli ,wakianza safari yao kupitia lango la Kilema ,aina
hi ya utalii ikiwa ni bidhaa mpya katika Milima huo mrefu kuliko yote
barani Afrika.
Aina
hii mpya ya utalii ambayo kwa sasa imeanza kushika kasi katika Hifadhi
za Taifa ,za Mlima Kilimanjaro,Arusha na Saadan inatokana na Shirika la
Hifadhi za Taifa (TANAPA) kuendelea kupanua wigo wa vivutio katika
Hifadhi zake 16,
Meneja
Mawasiliano na Mahusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal
Shelutete amesema hatua ya Juanito na wenzake kufika katika kilele cha
Uhuru inaashiria kuanza kufunguka kwa aina hii mpya ya utalii katika
Hifadhi za Taifa .
Shelutete
amesema namna ambavyo Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) limekuwa
mstari wa mbele katika kubuni aina mpya ya bidhaa za utalii ili
kushindana na nchi nyingine duniani katika uuzaji wa safari kwa watalii.
Kwa
upande wake Juanito Oiarzabal ambaye amepata ulemavu wa kukatika vidole
kutokana na barafu katika Milima mbalimbali aliyopanda amesema
changamoto aliyokutana nayowakati wa kupanda mlima ni kuzoea hali ya
hewa yam lima ambayo imekuwa ikibadilika kila mara.
Mkurugenzi
wa kampuni ya Safari Bike Africa iliyoratibu changamoto ya kupanda
Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli kwa wageni hao,Mario Martos
amesema kampuni yake imekusudia kuleta mabadiliko katika sekta ya utalii
kwa kufanikisha safari za watalii wa kutumia baiskeli.
Shirika
la Hifdhi za Taifa (TANAPA) limejipanga kuhakikisha usalama wa hali ya
juu kwa wageni watakaofanya aina hii mpya ya utalii katika Hifadhi zake
kwa kuwa na taahadhari sambamba na waongoza wageni waliobobea katika
kazi ya Utalii.
No comments:
Post a Comment