Mbunge wa Segerea Mh. Bonnah Kaluwa akisalimiana na wachezaji wa timu ya Bodaboda Kimanga kabla ya mchezo wa fainali
Mbunge wa Segerea Mh. Bonnah Kaluwa katika picha ya pamoja na EFM jogging club
Mheshimiwa Bonnah Kaluwa akionyesha umahiri wa kupiga danadana akitazamwa na wachezaji wa zamani wa Taifa Stars
Mshambuliaji wa timu ya Sigara FC akijaribu kuwatoka mabeki wa Bodaboda
Mamia ya mashabiki wakifuatilia mchezo
Mheshimiwa Bonnah Kaluwa akiungana na mashabiki kucheza singeli
Mkali wa muziki wa Singeli Msaga Sumu akiwaburudisha mashabiki waliojitokeza kwa wingi
Mbunge wa Segerea Mh. Bonnah Kaluwa amejumuika
na wakazi wa jimbo lake katika bonanza lilijomuisha michezo mbalimbali.
Bonanza hilo lililofanyika katika uwanja wa Sigara uliopo Tabata
lilikuwa ni hitimisho la mashindano ya Bonnah Cup 2017 ambapo fainali
ilikuwa ni kati ya Kimanga Bodaboda na Sigara FC huku timu ya Bodaboda
ikiibuka kidedea kwa mikwaju ya penati 5-4.
Mshindi wa fainali alijishindia shilingi
milioni moja taslimu pamoja na pikipiki wakati mshindi wa pili akipata
shilingi laki tano na mshindi wa tatu akiondoka na shilingi laki tatu.
Akizungumza baada ya fainali
Mheshimiwa Bonnah Kaluwa amesema mashindano hayo yatakuwa endelevu kila
mwisho wa mwaka ili kuinua michezo jimboni hapo na kusema mshindi wa
mwaka huu atapata nafasi ya kwenda Dodoma kushindana na timu ya wabunge.
No comments:
Post a Comment