Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Joseph Kakunda akipanda ngazi kukagua mradi wa maji kijiji cha Eworendeke Kata ya Kimokouwa wilayani Longido. |
Mhe Joseph Kakunda na Mkuu wa wilaya ya Longido,Godfrey Chongolo wakijumuika na wananchi kuimba wimbo wa kufurahia mradi wa maji. |
Mhe Joseph Kakunda na Mkuu wa wilaya ya Longido,Godfrey Chongolo wakiagana na wananchi wa Kijiji cha Ranchi. |
Na Mwandishi Wetu,Arusha
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za
Mitaa(Tamisemi),Joseph Kakunda amepongeza ujenzi wa miradi ya maji
inayotekelezwa katika mpango wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya
Tabia Nchi katika wilaya za Longido,Monduli na Ngorongoro.
Mradi huo unaosimamiwa kwa pamoja na
Ofisi ya Rais-Tamisemi,taasisi ya kimataifa ya maendeleo na
mazingira(IIED) na Haki Kazi Catalyst unatarajiwa kuwanufaisha wananchi
walio katika wilaya hizo tatu.
Akiwa katika Kijiji cha Eworendeke Kata ya Kimokouwa alipongeza hatua iliyofikiwa ya kuwawezesha wananchi kupata maji safi kwaajili ya matumizi ya nyumbani pamoja na mifugo yao ikizingatiwa wilaya ya Longido asilimia 95 ya wakazi wake ni wafugaji.
Amesema mkandarasi amekua mzalendo kwa kujenga miundombinu ya maji tenki pamoja eneo la kunyweshea mifugo kwa thamani ya Sh 36 milioni na kuonya wakandarasi wasio na uzalendo wanatekeleza miradi kwa gharama kubwa lakini inakua haina ufanisi.
Mkuu wa wilaya ya Longido,Godfrey Chongolo amesema wilaya yake ipo jumla ya miradi 14 inayofadhiliwa na IIED kwa lengo la kuwawezesha wananchi kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Naye Flora Assey ambaye ni mratibu wa mradi huo kutoka Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha amesema lengo la mradi huo ni kuweka mfumo utakaowezesha upimaji wa kiutendaji katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Imeandaliwa na mtandao wa www.rweyemamuinfo.blogspot.com
No comments:
Post a Comment