Baadhi ya Watalii wakishuka kutoka
kwenye meli ya kitalii ya kampuni ya Nautica
Majuro katika Bandari ya Dar es Salaam.
Mtalii wakipiga picha “Selfie” punde baada
ya kuwalisili katika Bandari ya Dar es Salaam.
Mtalii akicheza ngoma baada kunogewa na
mrindimo wa ngoma ya utamaduni wa
Tanzania.
Bodi ya Utalii Tanzania imeshiki kutoa taarifa za utalii wa Tanzania kwa watalii
takribani 570 waliowasili kwa meli ya kitalii
ya kampuni ya Nautical Majuro katika
Bandari ya Dar es Salaam .
Ujio wa Meli hii ya
kitalii ni mwendelezo wa juhudi
zinazofanywa kwa kushirikiana na wadau wa
Utalii wa Tanzania kwa dhamira ya
kuwajulisha watalii kutoka katika nchi
mbalimbali duniani kuwa wanaweza kuja
kuvitembelea vivutio vya utalii vya Tanzania
kwa kutumia njia mbali mbali za usafiri (meli,
ndege na njia ya barabara).
Watalii hawa wameweza kutembelea Pori la
Akiba la Selous, eneo la Mlima Kilimanjaro,
Mji wa Kihistoria wa Bagamoyo na jiji la Dar
es Salaam.
Meli hii imeanza safari zake katika bara la
ulaya imewasili Tanzania tarehe 2/01/2018
saa 2 asubuhi na kuondoka saa moja usiku.
No comments:
Post a Comment