Mkurugenzi
wa Tasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi akiwa katika picha ya
pamoja wageni waalikwa wakiwa wameshika kitabu kidogo kinachozungumzia
haki na mambo mbalimbali ya haki za watoto.
Mkurugenzi wa Tasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kitabu Kidogo kinachozungumzia haki na mambo mbalimbali y watoto na kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.
Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Tamwa, Valerie Msoka akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika Protea Jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria aliyoongoza jopo la Mawakili kupinga sheria ya ndoa za Utotoni katika Mahakama kuu ya Tanzania.
Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Msichana Initiative,Benedict Kikove akitoa neno la shukrani kwa wadau waliofika katika uzinduzi wa kijitabu cha sheria ya kupinga ndoa za utotoni.
Baadhi ya wadau waliofika kushuhudia uzinduzi wa Kitabu Kidogo kinachozungumzia haki mambo mbalimbali za watoto na kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.
Mkurugenzi wa Tasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi akiwa katika picha ya Pamoja na wadau wakati wa uzinduzi wa Kitabu Kidogo kinachozungumzia haki mambo mbalimbali za watoto na kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
TAASISI
ya Msichana Initiative imezindua kitabu kidogo kinachozungumzia haki
mbalimbali za watoto na kupinga ndoa za utotoni kwa mtoto wa kike.
Uzinduzi
wa kitabu hicho umefanyika leo jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa
tasisi hiyo Rebeca Gyumi amesema ni vema watanzania wakakitumia kitabu
hicho kilichoandaliwa na timu ya mawakili kwani kimeandikwa kwa lugha
rahisi zaidi kuhusu maamuzi yote yanayotolewa na Mahakama Kuu ya
Tanzania Julai 8 mwaka 2016.
“Mahakama
Kuu, kupitia Majaji wake katika kesi hii waliona kuwa vifungu hivi
haviendani na Katiba ya nchi.Pia vinabagua haki za watoto wa kike
ukilinganisha na haki za watoto wa kiume.
"Vifungu
hivyo vinaruhusu mtoto wa kiume kuoa katika umri wa miaka 18 na mtoto
wa kike kuoelewa katika umri wa miaka 14 na 15 kwa ruhusa ya Mahakama na
wazazi,"amesema Gyumi.
Amesema
vifungu hivyo vinachochea kwa kiasi kikubwa suala la ndoa za utotoni
hasa kwa watoto wa kike na kutaja Tanzania ni moja ya nchi yenye
asilimia kubwa ya tatizo la ndoa za utotoni ikilinganishwa na nchi
zingine za ukanda wa Afrika Mashariki ukiacha Uganda.
Ameongeza
wasichana wawili kati ya watano huolewa kabla ya kufikia umri wa miaka
18 na wasichana hao hukumbwa na changamoto nyingi wanapoingia katika
ndoa.
"Wanaolewa
wakiwa na mri mdogo wanapopata mimba wakati wa kujifungua wanakuwa
kwenye hatari kubwa ya kupoteza maisha kwa sababu via vyao vya uzazi
bado ni vichanga.Pia huwanyima haki yao ya kupata elimu,"amesema.
Gymi
amesema kupitia kitabu hiki chenye maamuzi ya Mahakama Kuu, jamii
itaelewa na kutambua zaidi namna ambavyo vifungu hivyo kandamizi kwa
watoto wa kike na kuona haki ambazo zimetambuliwa kisheria kupitia
hukumu hiyo, pia madhara ya ndoa za utotoni .
Amefafanua
Msichana Initiative pamoja na wadau wengine wanaamini suala la ndoa za
utotoni litakoma endapo jamii itakuwa tayari kuwashika mkono watoto wa
kike kwa kuwalinda na kutetea haki zao msingi.
No comments:
Post a Comment