Umoja
wa Ulaya (EU) umeipatia serikali ya Tanzania msaada wa Euro Milioni 4.5
(Tsh. 12 Bilioni) ili kufanikisha miradi mikubwa mitatu ya sekta ya
kilimo ambayo inatekelezwa kupitia Mpango wa Kuendeleza Kilimo Ukanda wa
Kusini mwa Tanzania (SAGCOT).
Miradi hiyo itatekelezwa katika mikoa ya Iringa, Morogoro ambapo itafanyika miradi miwili.
Akizungumza
kuhusu msaada huo, Naibu Waziri wa Kilimo, Mary Mwanjelwa alisema
msaada huo utasaidia wakulima wadogo kuboresha kilimo chao na kuwa cha
kibiashara zaidi kuliko sasa.
Mwanjelwa
alisema pamoja na kuwanufaisha wakulima, pia kama nchi itanufaika
kutokana na biashara itakayokuwa ikifanyika jambo ambalo litasaidia
uchumi wa nchi kukua.
“Wamekusudia
kufufua kilimo cha kisasa, kilimo bora ili Watanzania wanufaike na
kilimo kwa kuwa na soko. Faida yake ni upatikanaji wa chakula, lishe na
biashara na mwisho wa siku wananchi wote wanufaike,” alisema Mwanjelwa.
Kwa
upande wa Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini, Roeland Van de Geer
alisema EU imedhamiia kusaidia mirad mingi hapa nchini katika sekta ya
chakula ili kuhakikisha kuwa jamii ya Tanzania inakuwa na chakula cha
kutosha.
No comments:
Post a Comment