Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas,akizungumza na Maafisa Habari, Asasi za Kiraia pamoja na waandishi wa habari
wakati kupokea taarifa ya mrejesho wa utafiti uloiofanywa na MISA Tanzania kwa kushirikiana na CIPESA
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MISA Tanzania Bw. Gasirigwa Sengiyumva akiuliza maswali wakati wa mapitio ya ripoti ya upatikanaji
wa Taarifa Tanzania uliofanywa na Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini
mwa Afrika(MISATAN) ikishirikiana na Taasisi ya CIPESA ya nchini Uganda.
Wakili
wa Mahakama Kuu Tanzania Bw. James Marenga akitoa mrejesho wa utafiti
uloiofanywa na MISA Tanzania kwa kushirikiana na CIPESA kwa Maafisa
Habari wa Serikali, Asasi za Kiraia pamoja na Waandishi wa Habari Jijini
Arusha.
Bi.
Ashnah Kalemera kutoka CIPESA akiwasilisha mambo mbalimbali
yanayohusiana na upatikanaji wa Taarifa katika ukanda wa Afrika
Mashariki
Bi.
Juliet Nanfuka kutoka CIPESA akizungumza jambo wakati wa kupokea
taarifa ya utafiti iliyofanywa na MISA Tanzania kwa kushirikiana na
CIPESA
Baadhi ya wadau mbàlimbali pamoja na waandishi katika mkutano huo
Mwandishi wa Gazeti la Habari leo Veronica Mheta akichangia mada katika mkutano huo
Mwenyekiti
wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw. Paschal
Shelutete akijibu maswali mbalimbali wakati wa mapitio ya ripoti ya
upatikanaji
wa Taarifa Tanzania uliofanywa na Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini
mwa Afrika(MISATAN) ikishirikiana na Taasisi ya CIPESA ya nchini Uganda
Kaimu
mkurugenzi wa MISATAN nchini Gasirigwa Sengiyumva (wa kwanza
kushoto)akiwa na mmiliki wa Wazalendo Blog,Gadiola Emmanuel (mwenye
skafu nyekundu shingoni) wakati wa kusikiliza wadau wanatarajia nini baada ya kusikiliza ripoti ya utafiti.
Mwenyekiti
wa MISA Tanzania Bi. Salome Kitomari akitoa neno la Shukurani ikiwa ni
pamoja na kumshukuru Msemaji Mkuu wa Serikali Hassan Abbas kwa ushiriki
wake,Maafisa habari mbalimbali wa Serikali, Wadau kutoka Asasi za Kiraia
pamoja na waandishi wa Habari.
Mafunzo yakiendelea katika Hotel ya Impala Jijini Arusha.
Na.Vero Ignatus Arusha.
MSEMAJI
Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas amesema Maafisa Mawasiliano
serikalini bado wanakabiliwa na changamoto kutoka kwa mabosi wao,
ikiwano wengine kutokutaka habari zao zisikike kwenye vyombo vya habari.
Dkt.Abbas
aliyasema hayo jana mjini hapa wakati mapitio ya ripoti ya upatikanaji
wa Taarifa Tanzania uliofanywa na Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini
mwa Afrika(MISATAN) ikishirikiana na Taasisi ya CIPESA ya nchini Uganda.
Alisema
kupitia ripoti hiyo aliyoiunga mkono na kuisoma vyema atahakikisha
maofisa mawasiliano zaidi ya 300 wanaokutana mjini Arusha wanapata
utafiti huo."Nimesoma
utafiti huu, kurasa zote upo vizuri, niwaombe muendelee kufanya tafiti
kama hizi kwani ni chakula kwetu," alisema Dkt. Abbas.
Akizungumzia
utafiti uliofanywa katika mikoa 7 na MISATAN Wakili wa mahakama kuu
James Marenga amesema ofisi za halmashauri ya mikoa ya Arusha na kigoma
,walau ndiyo zimeonekana ndiyo wanafanaya vizuri katika kuwa wazi katika
utoaji wa taarifa kuliko ofisi za mikoa.
Dodoma
manispaa,halmashauri ya Jiji la mbeya,Kigoma ofisi ya mkuu Arusha,
ofisi ya mkuu wa mkoa Mwanza hakukuwa na ushirikiano,vilevile mkoa wa
Mtwara hakukuwa na ushirikiano ,Dar ni katika halmashari ya Jiji,Kwahiyo
Utafiti huo ulikuwa umegawanya utoaji wa taarifa kwa ofisi za mkuu wa
mikoa na ofisi za halmashauri au za Majiji katika mikoa iliyochaguliwa.
Moja
ya mapendekezo yaliyotolewa baada ya utafiti huo vitengo vya watoa
taarifa vinaimarishwa kama inavyotakiwa katika sheria ya haki kupata
taarifa ya mwaka 2016.Vilevile utafiti huo unasisitiza kuwepo na uwazi
katika utoaji wa taarifa haswa kwenye taasisi za serikali.
No comments:
Post a Comment