Social Icons

Monday, 19 March 2018

FASTJET YAWEZESHA MADAKTARI KUSAFIRI KUTOA HUDUMA YA AFYA YA KINYWA NA MENO BURE KWA WANANCHI WILAYANI TARIME

 AQ6A7818.jpg
 Baadhi ya Madaktari watoa huduma ya meno na kimywa  pamoja na  watumishi wa Fastjet wakiwa wamewasili jijini Mwanza wakitokea Dar es salaam.

 AQ6A7930.jpg
 AQ6A7945.jpg
 Madaktari kutoka chama cha madaktari wa kinywa na meno Tanzania wakiwa wilayani tarime mkoa wa mara kuendelea kutoa elimu ya kinywa na meno ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya afya ya kinywa na meno Duniani, ambapo walikuwa wanatoa huduma za uchunguzi,matibabu na elimu kwa wakazi wa wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kuwafikia wanafunzi na watoto yatima.AQ6A7949.jpg
Msemaji wa Fastjet Tanzania Bi. Lucy Mbogoro akiwapatia wanafunzi dawa za mswaki pamoja na miswaki kwa ajili ya kuendelea kuweka meno yao safi pamoja na vinywa vyao.
 AQ6A7959.jpg
Mmoja wa madakrtari wa meno na kinywa akiendelea kutoa elimu kwa wanafunzi.
AQ6A8009.jpg
Mh. Mariam  Mkono, Diwani wa Viti Maalum akizungumza na madaktari wa kinywa na meno kijijini Nyamwaga. 
 AQ6A8014.jpg
Debora Magasi, Muuguzi Mkuu wa hospitali ya Halmashauri ya Wilaya akizungumza na madaktari wa kinywa na meno kijijini Nyamwaga
AQ6A8020.jpg
Mganga Mkuu wa Kinywa na Meno wa Mkoawa Mara, Dkt Nila Jackson, alisema kati ya Machi 13 hadi 16 mwaka huu madaktari hao walifikia jumla ya wananchi 710  katika kijiji cha Nyamwaga wakiwemo wanafunzi 510 kutoka shule za msingi saba kijijini humo.
AQ6A8024.jpg

Raiswa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania Dkt. Ambege Jack Mwakatobe, alitoa wito kwa madaktari wa mikoa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi angalau mara mbili kwa mwezi ili kuwaongezea ufahamu na uelewa wananchi juu yausafi wa kinywa.

***********
SHIRIKA la Ndege la Fastjet limewezesha Madaktari wa kinywa na meno kusafiri kwenda kutoa huduma ya afya ya kinywa na meno bure kwa wananchi wa wilaya ni Tarime mkoani Mara.



Madaktari kutokachama cha madaktari wa kinywa na meno Tanzania wameanza ziara ya kujitolea katika wilaya ya Tarime mkoani mara ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya afya ya kinywa na meno duniani ambapo watatoa huduma zauchunguzi, matibabu na elimu kwa wakazi wa wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kuwafikia wanafunzi na watoto yatima.



Akizungumza hivi karibuni wilayani Tarime, Daktari wa Meno wa Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Dk. David Mapunda, alisema ziara hiyo itawapatia fursa madaktari hao kufanya uchunguzi wa kinywa pamoja na kutoa huduma za matibabu pamoja na elimu kwa wakazi wa wilaya hiyo.

Alisema miongoni mwa magonjwa yanayosumbua katika kinywa ni pamoja nakuoza kwa meno na ugonjwa wa fizi ambayo yanasababishwa na uchafu unaotokana na kutokupiga mswaki, kukosea kupiga mswaki au kutumia mswakiusio faa.

Alisema ili wananchi waepukane na magonjwa hayo ya meno wanapaswa kupiga mswaki angalau mara mbili kwa siku na kujenga utaratibu wa kuangalia afya ya kinywa na meno mara kwa mara.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Kinywa na Meno wa Mkoawa Mara, Dkt Nila Jackson, alisema kati ya Machi13 hadi 16 mwaka huu madaktari hao walifikia jumla ya wananchi 710 katika kijiji cha Nyamwaga wakiwemo wanafunzi 510 kutoka shule zamsingi saba kijijini humo.

"Kati ya tarehe hizo Madaktari hao  walitoa uchunguzi, matibabu na elimu ya afya ya kinywa na meno na kati ya tarehe 17 hadi 20 watakuwa katika wilaya ya Tarime na Rorya kuendelea na zoezi hilo," aliongeza Dk.Jackson

Naye Raiswa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (Tanzania Dental Association), Dkt. Ambege Jack Mwakatobe, alitaja kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya kinywa na meno Duniani inayosema “Sema ah, fikiri akinywa, fikiria afya” ambayo inalenga kuwahamasisha wananchi kuzingatia afya ya kinywa na meno ilikujikinga na magonjwa yanayohusiana na ugonjwa wa meno ikiwemo magonjwa yakisukari na mengine.

Aidha alitoa wito kwa madaktari wa mikoa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi angalau mara mbili kwa mwezi ili kuwaongezea ufahamu na uelewa wananchi juu ya usafi wa kinywa.

Akizungumza kutoka kijiji cha Nyamwaga, Msemaji wafastjet nchini, Lucy Mbogoro,  alisema shirika la fastjet linafuraha kuwa sehemu ya shughuli hii inayofanywa na madaktari hawa wazalendo.

"Shirika la fastjet limewawezesha madaktari hawa kusafirikutoka Dar es salaam hadi Mwanza na kurudi ikiwa ni sehemu yampango wake wakurudisha shukrani kwajamii," alisema.

 

No comments: