"Shemeji
zangu walikuwa sita walinipiga sana kwa kweli kwa sababu ya kutaka
kumiliki Mali za Mume wangu ambaye ni Marehemu" , ni mmoja ya wanawake
wa Tarime akisimlia kwa masikitiko kutokana na ukatili alioupata baada
ya kufiwa na mumewe, ambapo ndugu wa mume alilazimisha kumrithi yeye na
mali za mumewe. Mila kama hizi zinazomkandamiza mwanamke zinapaswa
kusitishwa
"Tumekubali
kabisa watoto wetu wa kike wasiendelee kukeketwa ,lakini bado jamii
zetu hazituelewi tunaendelea kuwaelimisha ili nao wabadilike."- Mzee wa
Kimila (Aliyesimama). Bado kuna kazi kubwa ya kumaliza swala la
ukeketaji lakini kupitia elimu mbalimbali na mafunzo yanayotelewa kuhusu
maswala ya ukeketaji juu ya hasara na madhara yake inaendelea kupunguza
idadi ya wanaokeketwa.
"Kwa
Tarime mwanamke kupigwa na kuvuliwa nguo hadhalani ilikuwa ni kitendo
cha kawaida tu" - Sara Boniface (aliyesimama) , alielezea kwa kina
kuhusu ukatili wa kupigwa ambapo aliongeza kwamba kwa sasa ukatili huo
umepungua kutokana na elimu wanayoipata wanajamii juu ya ukatili wa
kijinsia.
Mmoja
wa wazee wa Kimira kutoka Tarime(aliyesimama) akieleza juu ya ukeketaji
na kudai kuwa mwanamke aliyekeketwa anakuwa na thamani kubwa kama
ilivyo kwa mwanamke mweupe kwa wasukuma, hii ni moja ya sababu
zinazosababisha ukeketaji uendelee. Ikiwa elimu itaendelea kutolewa
ukeketaji huu utapungua kwa kiasi kikubwa.
"Ukatili
wa ukeketaji ulikuwa unafanyika hadharani kweupe, wazazi walikuwa
wanalazimisha mabinti zao kukeketwa ili wapate mahali nyingi zaidi,
ambapo fedha hizo ziwasaidie katika kupata kipato zaidi" - Nyakerandi
Mariba. Swala hili limepungua sana kutokana na juhudi za wanamabadiliko
kuendelea kutoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia.
"Maswala
ya ukatili wa kijinsia yanaleta madhara makubwa katika jamii zetu,hasa
kwa mabinti na akina mama"-Lucy Matemba Afisa maendeleo ya jamii Tarime
Meneja wa kampeni ya Tunaweza Bi. Eunice Mayengela akiendelea kutoa Muongozo wa majadiliano
Wanamabadiliko wakiendelea kufuatilia mjadala
"Kila
wiki tunapokea kesi zaidi ya kumi (10) zanazoripotiwa Tarime zikihusu
kipigo,ubakaji, ulawiti na wanawake kutishiwa kuuwa,kupigwa sana kisha
kubakwa kwa lazima ama kulawitiwa"- Dawati la Jinsia . Licha ya kesi
hizo kuwa nyingi lakini elimu inayoendelea kutolewa na kampeni ya
tunaweza imesaidia sana kupunguza ukatili wa kijinsia.
Wazee wa Kimila kutoka Tarime wakiteta jambo wakati wa mjadala
Wanamabadiliko wakiwa katika picha ya pamoja.
Picha na Fredy Njeje
No comments:
Post a Comment