Social Icons

Tuesday 17 April 2012

Leo ni Kumbu kumbu ya Mzee wetu Anthony Simon Njeje ambae anatimiza Miaka mi nne Tangu alipo Fariki 17.04.2008 pamoja na matukio mbali mbali.

Marehemu Anthony Simon Njeje Enzi za uhai wake 
Marehemu Anthony S Njeje Akiwa na Familia yake enzi za uhai wake, yeye ni wa kwanza kushoto, Akifuatiwa na Dada wa kwanza Aninziye Njeje, Mama, Mtoto wa pili Ernest Luseshelo, na mimi Mwenyewe Fredy Njeje wakati nikifanya mahafari ya kumaliza Shahada ya kwanza.
 Hii ni Picha ya msalaba wa Marehemu
 Picha ambayo ipo katika Kaburi la Marehemu 
Picha ya Mama kushoto, Aliye chuchumaa anaitwa Sarehe na mimi tulipo tembelea Kaburi la marehemu


Sillas Mbuya siku alipo Tembelea Kaburi la Marehemu 
 Anthony JR akiwa na Mdogo wake Shikunzi siku walipo Tembelea kaburi la babu yao
 Mtoto Mkubwa wa Marehemu Aninziye Njeje akiwa na Mtoto wake Yasinta siku walipo tembelea Kaburi la Marehemu
 Kutoka Kushoto ni Ernest Luseshelo Njeje akiwa amempakata Alvin na Antony Jr, anaefuatia ni Aninziye akiwa amempakata Yasinta, wa tatu ni Shangazi Dada wa Marehemu akiwa amempakata Amerisa na wa mwisho ni Sarah Sichalwe Njeje. Walipo tembelea kaburi la marehemu
 *********

Ni miaka minne sasa imepita tangu ulipo enda kwenye makao ya kudumu.Hatupo nawe kimwili lakinii kiroho upo nasi daima. Tunakukumbuka sana Baba yetu Mpendwa. Unakumbukwa sana na Mke wako Mpendwa Mama Elizabeth Anthony Njeje, Wanao Aninziye, Luseshelo-Ernest, Fredy na Sarah. Wajukuu zako Anthony Jr, Shikunzi-Alvin, Amarisa na Yasinta, Pia unakumbukwa na wafanyakazi wenzako, majirani zako, waumini wenzako, ndugu Jamaa na Marafiki. Sisi Tulikupenda sana lakinin Mungu alikupenda Zaidi. Jina la Bwana Libarikiwe.
AMEN



No comments: