Social Icons

Monday 7 May 2012

FRANCOIS HOLLANDE ASHINDA URAIS NCHINI UFARANSA HUKU SARKOZY AKIKUBALI MATOKEO.


Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa amekubali kushindwa katika awamu ya pili ya uchaguzi wa nafasi ya urais.
Kiongozi wa chama cha kisoshalisti Francois Hollande amepata ushindi wa asilimia 51.7 ya kura dhidi ya asilimia 48.3 za Nicolas Sarkozy.
Akihutubia wafuasi wake baada ya ushindi, Francois Hollande amesema kuchaguliwa kwake kunaonyesha kuwa raia wa Ulaya hawaridhiki na hatua za kubana matumizi katika kupambana na mgogoro wa kifedha na kuwa sera za kukaza mkanda haziwezi kuwa suluhisho pekee kwa mgogoro huo.
Rais Barack Obama wa Marekani ni miongoni mwa viongozi wengi wa mataifa duniani waliompigia simu Hollande na kumpongeza kwa ushindi alioupata.
Sarkozy ataingia katika historia kuwa kiongozi wa kwanza  wa Ufaransa kushindwa baada ya kuongoza muhula mmoja tu. 

No comments: