Social Icons

Monday, 21 May 2012

Mastaa wa Bongo: Mahusiano kati ya Diamond na Mrembo Jokate yaingia Kasoro ni Baada ya kupatikana taarifa alikuwa na Aunt Ezekiel



Naseeb Abdul ‘Diamond’.
Jokate.
Stori: Musa Mateja na Shakoor Jongo
KITENDO cha hivi karibuni cha mwanamuziki Naseeb Abdul ‘Diamond’ kunaswa hotelini na staa wa filamu za Kitanzania, Aunt Ezekiel, kumetibua mambo na sasa inadaiwa uhusiano wa kimapenzi wa kidume huyo na mwanamitindo Jokate Mwegelo umeingia mdudu mbaya, Ijumaa Wikienda lina mkanda mzima.
Chanzo cha kuaminika kilichoomba jina liwekwe kapuni kimedai kuwa tangu kuzagaa kwa habari za Aunt na Diamond kubambwa katika Hoteli ya Kebby’s iliyopo Mwenge, Dar wakila ‘good time’, Jokate anadaiwa kumaindi na kumnunia mwanamuziki huyo kiwango.
“Kwa kifupi Diamond na Jokate kimeshanuka. Jokate tangu asikie tetesi hizo kisha kusoma kwenye gazeti, hapokei simu za mpenzi wake huyo. Diamond atakuwa na kazi ya kumbembeleza ili kumrudisha kwenye hali ya kawaida,” kilidai chanzo hicho.
Katika kutafuta mzani wa habari hiyo, Ijumaa Wikienda lilifanya jitihada za kuwatafuta wahusika na Diamond alipopatikana alifunguka nusunusu:
“Aaah!Hakuna kitu kama hicho bwana (anacheka), mbona mambo yako sawa tu, ila sasa hivi simu yangu inasumbua, nitafute baadaye nitakupa ukweli.”
Hata hivyo, alipotafutwa baadaye aliendelea kuchenga kutoa ufafanuzi juu ya suala hilo, mazingira yaliyoashiria kuna kitu ambacho hakupenda jamii ikijue kwa sasa.
Baada ya Diamond kuchenga kuzungumzia uhusiano wake ulivyo kwa sasa, Jokate kwa upande wake alionesha kuwa na kitu moyoni na mahojiano kati yake na mwandishi wetu yalikuwa hivi;
Mwandishi: Mambo Jokate?
Jokate: Safi za siku?
Mwandishi: Ni nzuri tu, vipi hali yako zaidi?
Jokate: Mimi niko poa. 
Mwandishi: Kuna habari tumezinasa kuwa sasa hivi huongei na mpenzi wako Diamond kisa kunaswa na Aunt, ni kweli?
Jokate: Hahaaa… duh.. bwanaa! Mimi sitaki.
Mwandishi: Hutaki nini sasa?
Jokate: Sitaki tu udaku.
Mwandishi: Siyo udaku ila nimekuuliza swali, unatakiwa ujibu, unaongeleaje sakata hilo kwa jumla?


No comments: