Ni kitambo sasa tangu kuwepo kwa taarifa kuwa staa wa Bongo Movie, Juma Kilowoko, 'Sajuki' ni mgonjwa , huku pia taaraifa za karibunu zikidai kuwa hali ya nyota huyo bado ni tete na kuzua hofu kubwa kwa mashabiki wake.
Kupitia teeentez.com pekee taaraifa rasmi ni kuwa hali nyota huyo kwa sasa ni njema yuko tayari tena kuanza kuwatumikia watanzania kupitia tasnia ya filamu.
Kwenye Exclusive interview aliyofanya na teentz.com mapema leo Sajuki amewashukuru watanzania kwa kuwa pamoja nae kwenye wakati wote wa matatizo mpaka sasa anajisikia yuko vizuri tofauti na ilivyokuwa awali.
Nashukuru kuwa sasa niko poa, watanzania waelewe hilo, kwa sasa naweza hata kuendesha gari na karibuni nitaanza kucheza muvi tena alisema Sajuki.
katika kuonyesha kuwa anathamini mchango wa Watanzania Sajuki ameachia ngoma ambayo ameamua kuipa jinala Shukurani
No comments:
Post a Comment