Social Icons

Thursday 19 June 2014

LEO KATIKA MAHUSIANO: UJUE UTAPELI WA WANAWAKE KWA STAILI YA ‘NNA MIMBA YAKO DEAR’! SOMA HAPA UELEWE SIO UNAAMBIWA BBY NAMIMBA YAKO UNATUMBUA MACHO KA CHURA.



KABLA ya kwenda mbali naomba nikuusie wewe msomaji wangu juu ya kujiweka mbali na tabia ya kumdanganya mpenzi wako. Unapomdanganya mara moja, akigundua utakuwa umejipunguzia uaminifu na mapenzi lazima yatapungua.

Naamini ujumbe umefika kwa wale wenye tabia ya kudanganya hata pale ambapo hakuna ulazima wa kufanya hivyo. Nigeukie sasa kwenye mada yangu ya wiki hii. Mpenzi msomaji wangu, wapo wanawake ambao ni wasanii sana, wanatumia miili yao kujipatia pesa kwa njia wanazozijua wao.

Ukiwa na bahati mbaya, ukatokea kumpenda msichana ambaye ni msanii utaumia sana na inawezekana mpaka pale utakapokuja kuamua kwamba bora umuache, atakuwa amekuchuna kupita kiasi.

Nimtolee mfano dada mmoja anayeitwa Ashura Matashititi ambaye katika Jiji la Dar ni maarufu maeneo mbalimbali. Umaarufu wake umekuja kutokana na matukio yake. Amekuwa na wapenzi tofauti wa maeneo mbalimbali. Tabia yake kubwa ni kubambikia wanaume mimba.

Yaani leo akitembea na mwanaume f’lani, baada ya muda humwambia hajaziona siku zake na anahisi ameshanasa. Anaposema hivyo, hamaanishi ila anataka kutumia mbinu hiyo kupata pesa.
Meseji anayoweza kumtumia mwanaume aliyetembea naye inaweza kuwa imeandikwa hivi: “Dear mwenzio sijaziona siku zangu na nahisi nimenasa. Mbaya zaidi mama akisikia nina ujauzito nyumbani hapatakalika sasa tufanyeje?”

Msichana huyo ataandika hivyo akijua kabisa mwanaume ambaye alitembea naye siku kadhaa nyuma kwanza hana mpango wa kumuoa lakini pia hahitaji mtoto kwa muda huo.
Kwa maana hiyo jibu ambalo linatarajiwa kutoka kwa mwanaume huyo kwenda kwa binti aliyetembea naye ni kwamba lazima waitoe mimba. Mwanaume akishagusia hilo tu ameshaibiwa. Kitakachofuata hapo ni mwanaume kutakiwa kutoa pesa ili mimba itolewe.

Kumbe hakuna cha mimba wala nini, msichana atapewa pesa hiyo na baada ya siku mbili atadai ameshaitoa na sasa anaendelea vizuri ila ametakiwa ale sana vitu vya kuongeza damu.
Hapo tena mwanaume atatoa pesa, lakini msichana huyo atakuwa akizifanyia mambo yake kwani hakukuwa na suala la mimba hata kidogo.

Wanaume wengi wanaibiwa kwa njia hii na ukifuatilia sana utagundua kuwa wanaume wanaoingia kwenye uhusiano na wanawake wasio na penzi la dhati ndiyo wanaongoza kwa kufanyiwa hivi.
Hata hivyo, nimegundua kuwa wanaume wengi wanaibiwa kwa mtindo huu kutokana na mambo mawili. Kwanza, ulimbukeni wao. Kama uko kwenye uhusiano wa kawaida na mtu na hauko tayari kupata mtoto kwa muda huo, iweje ukubali kufanya mapenzi bila kinga?

Lakini ukiachilia mbali hilo la kutumia kinga, umetembea na mtu halafu baada ya muda anakuambia ana mimba yako kisha unakubali kirahisi na kumpa pesa nyingi akatoe. Una uhakika gani kama kweli ni mjamzito? Kama kweli ipo, umejiridhishaje kama ni yako?

Wengi wanaoshindwa kujiuliza maswali hayo ndiyo wanaoongoza kwa kulizwa na unakuta mwanaume anafanyiwa hivyo mara kibao halafu hashituki, hata kama ni ushamba, huu umepitiliza.

Lingine ni ubahili wa baadhi ya wanaume kwa wapenzi wao. Fuatilia utabaini kuwa wanawake wanaowafanyia wapenzi wao kamchezo hako ni ili wapate pesa kwa ajili ya kutatulia shida zao.
Inavyoaminika ni kwamba, kama mwanaume anazo na anampatiliza mpenzi wake hasa pale anapokuwa na shida, ni vigumu kufanyiwa hivyo. Atafanyiwaje wakati mwanamke anajua akiomba pesa utapewa?

Inavyoonekana hapa ni kwamba mchezo huu wanafanyiwa sana wale ambao wana pesa lakini wakiombwa na wapenzi wao wanakuwa wakali. Sasa dawa yao ni kudanganyiwa mimba na kwa kuwa wengi hawako tayari kupata mtoto, lazima watatoa pesa ikatolewe na pesa hiyo ndiyo inatumika kutatulia shida nyingine.

Jambo la tatu ni mwanaume kutokuwa na ‘future’. Hapa ni kwamba, kama kweli mtu anaingia kwenye uhusiano wa kawaida na msichana ambaye anampenda, ikitokea bahati mbaya mimba ikaingia, hawezi kufikiria ishu ya kuitoa.

Kwa maana hiyo wanaume wengi wanaolizwa ni wale ambao hawana mapenzi ya kweli, matokeo yake wakitamkiwa suala la mimba wako tayari kuteketeza fedha ili kiumbe kitakachowaunganisha kisiwepo. Hii ni mbaya sana!

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, kutoa mimba ni kosa na ni dhambi kwa Mwenyezi Mungu. Lakini pia niwashauri wanaume wenzangu kuwa makini na hawa wanawake wenye kamchezo haka ka’ kutafuta pesa kwa kudanganyia mimba.

Mbaya zaidi kuna hadi wake za watu ambao wanawaibia waume zao kwa mtindo huu. Utakuta wana mtoto mdogo, siku ya siku anadai ana mimba na kwa kuwa hawako tayari kuzaa na kwa kuwa mume ana mambo mengi, atatoa pesa ili mkewe akatoe mimba. Mke atachukua pesa, atakwenda kufanyia mambo yake. Hii siyo sawa kabisa!


GPL

No comments: