Social Icons

Sunday 11 December 2011

AIRTEL MONEY YAZINDULIWA RASNI MKOANI DODOMA JANA KWA SHANGWE

Mmoja wa sanii mahiri wa miondoko ya hip hop hapa bongo,Hamis
Mwinyjuma a.k.a Mwana FA akiwapagawisha baadhi ya wakazi wa mji wa
Dodoma waliofika jioni ya jana kwenye tamasha la uzinduzi wa huduma ya
Airtel Money,uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri,mjini Dodoma na
kuhudhuriwa na wati kibao
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Sir Juma Nature pichani
kati akishiriki uzinduzi wa Airtel Money ndani ya mji wa Dodoma jioni ya jana kwenye uwanja wa Jamhuri,ambapo watu mbalimbali walijitokeza kwa
wingi kulishuhudia tukio hilo adhimu,kulia ni Meneja Mawasiliano wa
kampuni ya Airtel, Jackson Mmbando na kushoto ni Meneja wa Airtel
Money-Tanzania,Asupya Bussi Nalingingwa
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wa kundi la Wanaume Halisi
kutoka TMK,likiongozwa na Juma Nature wakilishambulia jukwaa
vilivyo,kwenye tamasha la uzinduzi wa huduma ya Airtel Money,uliofanyika
jioni ya jana kwenye uwanja wa Jamhuri,mjini Dodoma na kuhudhuriwa na
wati kibao
Anajiita Simba Dume ndani ya msitu
mnene,ni mmoja ya Wasanii wakongwe wa hip hop hapa nchini,ndani ya
miondoko ya muziki wa kizazi kipya,Mfalme wa rhymes Afande Sele pichani
kati akiwa amezungukwa na washabiki wake,huku akiwaimbia wimbo wake wa
Karata Dume, shangwe na miluzi ikiwa imetawala uwanjani hapo jioni ya jana,wakati kampuni ya simu ya mikononi ya Airtel ilipokuwa ikizindua
huduma yake mpya ya Airtel Money kwa wakazi wa mji wa Dodoma jioni ya
leo
Namna shangwe za Aitel Money zilivyokuwa zikilindima usiku wa jana ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Pichani juu ni baadhi ya wakazi wa mji wa Dodoma waliojitokeza kwa
wingi jioni ya jana kwenye uwanja wa Jamhuri,wakati kampuni ya simu ya
Airtel,ilipokuwa ikizindua huduma yake ya Airtel Money,ambapo wakazi wa
mji huo wamejitokeza kwa wingi kwenye tukio hilo na kuipokea kwa shangwe
huduma hiyo.
Mmoja wa wasanii wa miondoko laini laini hivi,aitwaye Mr Blue
a.k.a Kabaisa akitumbuiza jukwaani jioni ya jana kwa wakazi wa mji wa
Dodoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la uzinduzi wa Airtel
Money
Q-Chilla a.k.a Savimbi akiwaimbisha washabiki wake jioni ya leo
kwenye uwanja wa Jamhuri wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel
Money

No comments: