Social Icons

Friday, 2 December 2011

Airtel yadhamini Umaskini Full Stop jijini Arusha, 20 percent afunika

Christina Shushu na Boniface Mwaitege kwa pamoja wakitoa burudani wakati wa semina ya Umaskini Fullstop iliyofanyika katika uwanja wa Sheikh Amani Abeid Arusha na kuhudhuriwa na umati mkubwa jijini hapo, wazungumzaji wakuu wa semina hii walikuwa ni Erick shigongo na James Mwang'amba chini ya udhamini wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel.
Waimbaji wa glorious Singers wakitumbuiza wakati wa semina ya umaskini Fullstop iliyodhaminiwa wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel na kufanyika katika uwanja wa Sheikh Amani Abeid Arusha ambapo wakazi wengi walijitokeza kupata mafunzo ya Ujasiliamali.
Mwanamuziki wa kizazi kipya 20 percent akitoa burudani wakati wa Semina ya umaskini fullstop iliyofanyika katika uwanja wa Sheikh Abeid Amani Arusha ambapo kampuni ya simu za mkononi ya Airtel walidhamini wa Semina hiyo kwa lengo la kusaidia vijana kuendelea kujiamini na kuajiri wenyewe kupitia mbinu mbalimbali za ujasiliamali.
Habari kwa hisani ya Mtaa kwa Mtaa Blog

No comments: