Rahmani Mpaka njia akipewa keki na Watangazaji wa Clouds FM kama zawadi yake na nyingine nyingi atakabidhiwa kama alivyo ahidiwa. Rahmani ni mtoto wa Marehemu Amina Chifupa na Mpaka Njia,kulia ni Babu yake ambaye ni baba yake marehemu Amina Chifupa amesindikizwa na mtoto Elleza (kati) ambaye ni mtoto wa mtangazaji Sakina Llyoka. Mtoto Rahman ametimiza miaka kumi leo sasa tangu kuzaliwa kwake.
Mnamkumbuka Bishanga Bashaija....! wakati ule wa mchezo wa kuigiza ulikuwa ukiitwa Mambo hayo,pichani kulia akifanya mahojiano mafupi na Watagazaji wa kipindi cha Leo Tena,pichani kati ni Zamaradi Mketema ambaye pia anatangaza kipindi cha muvi kiitwacho Take One.
Watangazaji wa Clouds FM/TV,Kulia ni Dina Marious,Sakina Lyoka,pamoja na Gea Habib.wakiruka Live kupitia Clouds TV.

Mmoja wa wasanii kutoka THT,ajulikanae kwa jina la kisanii Dogo Dito (pili kulia) akiongoza sala/dua ya kumuombea aliyekuwa Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Mr Ebbo,ambaye kwa sasa ni Marehemu (Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi), mbele ya baadhi ya Watangazaji wa Clouds FM/TV kwenye moja wapo ya studio za kituo hicho,zilizopo Mikocheni jijini Dar,ambapo matukio hayo mbalimbali yarushwa LIVE na Clouds TV.Kituo cha Clouds FM 88.4 pia kinasherehekea miaka 12 ya tangu kuanzishwa kwake.Pia tutakuwa tukiwaletea wageni waalikwa mbalimbali watakaokuwa wakifika kwenye kituo hicho kwa ajili ya kuzungumza machache kwa jamii mbalimbali.
No comments:
Post a Comment