Social Icons

Thursday 8 December 2011

JE HII NI SAWA KUTUMIA ALAMA ZA TAIFA KATIKA MATANGAZO YA FILAMU





Hii
ni moja ya Posters inayotangaza Filamu mpya ya Mr. president iliyochezwa
na Mchekeshaji, Stive Nyerere, ikiwa imebandikwa katika mitaa
mbalimbali ya jiji la Dar.

Kinachoshangaza
ni jinsi utumiwaji wa alama za Taifa kama Ngao ya Taifa na Bendera ya
Taifa vilivyopamba Posters hii Je kulikuwa na umuhimu gani wa kutumia
alama hizi katika matangazo ya Filamu hii?, hili ni moja kati ya maswali
yanayoulizwa na baadhi ya wadau wanaopata fulsa ya kugongana na Posters
hii mitaani.

2 comments:

Anonymous said...

mi naamini sio tatizo cause tunaiga kutoka kwa marekani na tumeshaona wakifanya hivyo mara nyingi tu

Bongo Film Data Base said...

Matumizi ya nembo hio ya taifa ni jambo la kawaida na sahihi kabisa tukizingatia kitengo cha uandishi na kiufundi wa uandaji filamu uliyo makini hasa hadithi aina za namna hiyo,tukiachilia mbali mambo ya hayo kwa upande wa pili vitu kama hivyo vinamshawishi na kumthibitishia mtu kitu kinacho zungumzwa humo ndani kweli kinahusiana na nyazifa hiyo wanayo izungumzia humo ndani na uhalisia unazisogelea fikra zetu.

Asinge weka alama ya aina yoyote ile inayoashiria au kuonesha kitu cha humo White House natumai napo watu tungekuwa na la kusema zaidi ya hilo....

Watanzania tuache kuwa watu wenye woga kiasi hicho na tena tukumbuke uwanja wa sanaa ndiyo sehemu sahihi isiyokuwa na mipaka ya kuikosoa na kuikumbusha serikali kama sio kiuelemisha kabisa..kupitia katuni za kwenye magazeti alama kama hizi si kitu kigeni kwenye mboni zetu.. na mfano mwingine iliyo wazi ni kazi za wenzetu kwenye mataifa yaliyo endelea kwenye uandaaji filamu na vitu vingine vya kisanaa kutumia alama na vitu vya serikali sitatizo kabisa tukianzia mageleza,vyombo vya kurekebishia sharia kama vituo vya polisi,jeshi, mahakama na la mwisho kabisa ni uwepo wa jengo linalofanana na White House bila kupungua jambo hata moja...

Big up kwa jopo zima lililoandaa MR PRESIDENT..(www.bongofilmdatabase.blogspot.com)