Social Icons

Wednesday, 7 December 2011

TAFAKARI KUHUSU ANTI-VIRUS AND VENEGA MOVEMENT

TUTAFAKARI..Tangu kumalizika kwa tamasha la kizalendo la kihistoria ambalo lilifanikiwa sana na kufungua ukurasa mpya kwenye tasnia ya sanaa kumeibuka mijadala mingi rasmi na isiyo rasmi ikiusisha dhana ya ANTIVIRUS na Vinega kwa ujumla..Mengi yanaongewa mtaani, ya kweri na yasiyo kweri,yaliyopo na yakutengenezwa,ya kujenga na yakubomoa,ya kimantiki na ya kishabiki lakini yote ni kudhihilisha kwamba watu wengi sasa wanafahamu kinachoendelea..Tuanze na siku ya tukio tarehe 26-11-2011,nilikuwa mitaa flani ya Mwenge baada ya kutoka kwenye mitkas yangu,nilikuwa nimepumzika joint flani ivi na washikaji tunapata mbili tatu mida ya kuanzia jioni,sio siri mda ule kila unapopita unasikia stori za ANTIVIRUS na VINEGA,baadae mida ya saa mbili usiku wakati bado tunavuta kasi za kuibuka pande za Ustawi,mara nikapigiwa simu na mchizi wangu"oyaa mwanangu uko wapi??uku Ustawi kimeshanuka vibaya,watu wameshona kama siafu,HAKUNA ATA NAFASI YA KU-PARK GARI na watu wanazidi kumiminika njoo usiuweke"..nilipofika eneo la tukio sikuamini ninacho kishuhudia,watu wengi,watu wamepandwa mzuka,watu wanafuraha isiyo kifani..kingine kilichonigusa ni aina zote na madaraja mbalimbali ya watu walikuwepo pale wanasiasa,mastaa,masela,watoto wa kishua,masista duu,wadau mbalimbali,mashefa nk wote wakionyesha nia moja tu WANASAPOT MABADILIKO..Niende kwa yaliyojili baada ya tukio:kila kona ilikuwa ni stori za Vinega kuwakalisha Clouds team,kuanzia blogs,magazeti,tvs,radios na haswa mitandao ya kijamii km hapa facebook..Kuna watu walikuja na mitazamo yao chanya na hasi..nitawaanika baadhi walioitoa hadharani.

No comments: