Social Icons

Saturday 10 December 2011

Wasanii wa Mizengwe waiuza KASH KASH wenyewe mitaani



Wakijadiliana na mteja ili wamuuzie DVD yao hiyo.






Mkwere nae akifanya ushawishi kwa wateja walau wanunue DVD hiyo.







Watu waliwazunguka na kuwashangaa lakini hapo hapo waliuza kazi yao.




Baada
ya kuona wasambazaji wa Filamu wengio ni mizingua na hujinufaisha wao
zaidi ya Msanii hwa jamaa wa MIZENGWE ambao ni manguli wa vichekesho
pale ITV wameamua kuingia mtaani wao wenyewe na kufanya umachinga wa
kuuza filamu yao.




Wasanii
hao kadha mbali na kufanya vyema katika vichekso vya kwenye Luninga
pale ITV pia wameunda kundi lao linalojulikana kama KASHA KASH.

Mara
kadhaa wamekuwa wakionekana katika mikusanyiko ya watu wakiuza filamu
yao hiyo na jana walibahatika kunasa wao wenyewe mbele ya Camera ya FK
BLOG na hatimaye kupata taswira hizi wakiwa katika Viwanja vya Julius
Nyerere almaarufu Sabasaba pale barabara ya Kilwa wakiuza Filamu yao
hiyo ya Kash Kash kwa watu waliofika kuangalia maonesho ya miaka 50 ya
Uhuru.



Hatua hii ya wasanii hawa ni ya kupongezwa maana wasanii wengi wamekuwa wakiibiwa haki zao na matapeli wachache.Habari Kwa Hisani ya Father Kidevu Blogu


No comments: