Social Icons

Wednesday, 18 April 2012

Tusipodhibiti Ujinga Dhidi Ya Freemasons Taifa Litaangamia


Picha hii imepigwa posta Dar es salaam.Ni mhubiri anyejifanya anazungumza dhidi ya freemason,lakini nadhani anaimarisha ujinga kuhusu dudu hili

Wapo watakaoona nakazania jambo dogo,wanapaswa kutafakari tena.sasa kila kona ya nchi hii,watu wajinga kwa waerevu,wasomi na wasiosoma,wakuu wa dini na wengi wengine waimba wimbo wa freemasons,jamii inaaminishwa hiki ni kikundi(dini)? ya kishetani inayoweza kusababisha kichawi ajali ili freemason wanywe damu za watu,eti wanaweza kuwapa watu utajiri kishetani,eti wanatawala dini zote kubwa,eti viongozi wote na watu wote maarufu ni wanafreemason,eti majengo yote makubwa kama kanisa la mtakatifu Petro Roma,Msikiti mkuu wa Makka,makao makuu ya Anglicana Cantebury,Umoja wa Mataifa,Umoja wa Ulaya,Umoja wa Afrika,ikulu za nchi zote,mabenki,mahospitali yana nembo za utambulisho wa uanachama wa freemason.UJINGA JUU YA UJINGA.Eti wanatumia ishara,vidole viwili "V" ,namna wanavyokumbatiana nk. UJINGA JUU YA UJINGA.Haki ya nani tutakuja kuambiwa hata tendo la ndoa ni ufreemason!!! nani atabaki??
  Hatari ya wazi ni kuwa Ujinga huu unaosambaa kwa uzushi kwa wajinga kuwaambia wajinga wenzao hata wasomi wanaoamini ujinga huu ni wajinga vilevile kwa sababu inawezekana kusoma habari za kweli juu ya freemason na kuelewa,sasa ni vipi wasomi uchwara wanaamini mizungu.hatari nyingine ni shambulio la imani za kidini.dini zote kubwa zimehusishwa na freemason,oooh mara papa wa wakatoliki na maaskofu hawa na wale ni freemasos,ooh mara makka kwenye kaaba kuna ishara ya freemasons,UJINGA JUU YA UJINGA. Hatri nyingine na iliyonifanya kuandika hii tafakari ni imani potofu kuwa freemason wanafanya mtu awe tajiri,nilipoandika mara ya kwanza hapa siku za nyuma kuna waliodhani ninajua juu ya freemason,walinipigia simu na hasa vijana wakiniuliza namna ya kujinga ili watajirike,siku nyingi baadaye juzi nimekutana na rafiki yangu wa siku nyingi mhitimi wa chuo kikuu,na sasa ni mwalimu kwenye chuo kikuu kimoja nchini,na anataka kugombea ubunge mwaka 2015,akanieleza anavyopanga kupata pesa za uchaguzi huo kuwa anatafuta uwezekano wa kujiunga na freemason sasa ili kufikia 2015 awe ameshakuwa tajiri.naam atakuwa mbunge gani huyu? anaamini ushirikina,kupata fedha za miujiza,ama kweli waafrika tumelaaniwa(ikubaliwe kwa ajil ya makala haya?
   Mhubiri huyu wa posta anongea ujinga wake mchana kweupe,anataja watu majina baadhi yao viongozi wa dini na serikali na kuwahusiha na ibada za shetani,anaendelea bila kuulizwa.tunajenga taifa la namna gani? wapo watu na magazeti kama jambo leo na tazama yanasaidia kueneza ujinga huu,hakuna anyelinda wasomaji wa habari tanzania? TUMEKWISHA
Na Ludovick
0715 927100   ,,0753927100

4 comments:

Anonymous said...

hatujakwisha naimani ya kuwa kwa pamoja tuyakemee haya kwa nguvu zetu zote na mungu asiyeyapenda haya atakuwa upande wetu

inshaallah

amin

Anonymous said...

inawezekana unajua unachokisema ingawa unakisema kinyume otherwise you don`t know what u are saying and for that i can say you are the great ignorant kuliko hata hao wanaoamini. for your information most things ulizomention hapo zinaexist and they are all set up to push only one agenda.so think thrice,do a research before u post anything otherwise kama unafanya kwa nia ya kuwarudisha watu kwenye giza hapo it`s okey. coz some genius said sometimes it`s better to stay in the dark...sorry kwa lugha ambayo nimetumia lakini na imani ujumbe umefika.

Anonymous said...

ni kweli usemalo, wameongeza chumvi sana juu ya freemason lakini yapo mengi yana ukweli. Ukiwa kama mwandishi hebu mtafute huyu mtu anaitwa Chande ambaye ni mtanzania kiongozi wa freemason hapa kwetu umhoji akupe ukweli na pia utafute kitabu chake alichoandika kinachoelezea ufreemason halafu utupe ukweli ili tuelewe maana tupo njia panda

Eng. Mahenge said...

Nakuunga mkono mwandishi wa makala hii, nikiionacho mimi ni kuwa mfumo wa kufikiri wa akili ya Waafrika wengi hasa Watanzanini imejengeka katika vitu vinavyoonekana na imamani, hali ambayo ni ya chini kabisa ya kufikiri. Wanaamini vitu wanavyoviona na kuvisikia bila kuhoji ukweli wake, nina mambo mengi ya kuandika hapa ila muda hauniruhusu. Lakini ukitaka kuthibitisha hilo angalia mfano, madhehebu yalivyo mengi hapa Tanzania, angalia watu walivyojaa Loliondo, angalia watu walivyoibiwa na jamaa wa DES, fikiria kuhusu mauuaji ya Albino na Vikongwe nk. Ni ukweli usiopingika kuwa watu wengi wanashabikia mambo ya free mason bila kujua undani wake. Ushauri wangu ni kuwa tujitahidi sana kujifunza na kuujua ukweli kama ulivyo na si kama unavyojitokeza, tusiwe watu wa kuamini kila tunachokiona na kusikia au kuhubiriwa.