Social Icons

Tuesday, 24 April 2012

Ubingwa Simba Waingia Kwikwi



 
Mshambuliaji wa timu ya Simba, Emmanuel Okwi (kulia) akipambana na
mchezaji wa timu ya Moro United, Omari Gae wakati wa mchezo wa Ligi Kuu
Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana.
Simba ilishinda mabao 3-0.Picha na Yusuf Badi
--
LICHA ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Moro United lakini ndoto za Simba jana
kutangaza ubingwa wa Ligi Kuu 2011/2012 ziliingia kwikwi baada ya
mechi ya Azam na Mtibwa Sugar iliyochezwa kwenye uwanja wa Chamazi,
kuvunjika.


Mechi hiyo ilivunjika baada ya wachezaji wa Mtibwa Sugar kugomea
penalti iliyotolewa na mwamuzi wa mechi, Rashid Msangi wa Dodoma kwenye
dakika ya 88 ya mchezo huo, wakati timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1.


Kwa hali hiyo kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka nchini (TFF), timu itakayovunja


mechi itapokwa pointi tatu na kupewa timu pinzani, hali
inayochelewesha sherehe za ubingwa za Simba kwani Azam ambayo jana
ilifikisha pointi 53 ina uwezo wa kufikisha pointi 59 zilizofikiwa na
Simba kama itashinda michezo yake miwili iliyobaki dhidi ya Kagera Sugar
na Toto Africans.


Ili Simba ijihakikishie kutwaa ubingwa inatakiwa kushinda mechi yake
ya mwisho Mei 5 dhidi ya Yanga ambapo itakuwa imefikisha pointi 62 au
ifikishe pointi 60 kwa kutoka sare, lakini ikifungwa, bingwa itabidi
aamuliwe kwa tofauti ya mabao kama ilivyokuwa msimu uliopita.


No comments: