Social Icons

Tuesday, 8 May 2012

MCHEZAJI WA KIMATAIFA WA SENEGAL BOCANDE AFARIKI DUNIA.


Mchezaji Soka wa kimataifa wa Senegal Jules-Francois Bocande (Pichani) amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 54.
Bocade amekuwa akiugua kwa miezi kadhaa baada ya kupata mshituko wa moyo na ameaga dunia baada ya kufanyiwa upasuaji.
Mchezaji huyo alivuma sana alipokuwa akicheza soka nchini Ufaransa mnamo miaka ya 80 ambapo alishiriki katika fainali tatu za kombe la mataifa ya Afrika akiwa nahodha wa timu ya taifa ya Senegal.
Mkuu wa Shirikisho la Soka la Senegal Augustin Senghor, amesema kifo cha Bocande ni pengo kubwa kwa Senegal, kwa kuwa alijitolea kikamilifu kwa nchi yake akitumia kipaji chake kwa juhudi kubwa.

No comments: