Social Icons

Friday 4 May 2012

MECHI KUCHANGIA TWIGA STARS SASA MEI 5


Mechi
maalumu ya hisani kwa ajili ya kuchangia timu ya Taifa ya wanawake
(Twiga Stars), kati ya timu hiyo na wasanii wa filamu maarufu kama Bongo
Movie sasa itachezwa kesho (Mei 5 mwaka huu).

Kwa
mujibu wa kampuni ya Edge Entertainment iliyoandaa mechi hiyo,
imerudishwa nyuma kwa siku moja kupisha mechi ya Yanga na Simba
itakayochezwa Jumapili.

Mechi
hiyo itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni
ambapo viingilio kwa viti vya rangi ya chungwa, kijani na bluu ni sh.
2,000, VIP C na B itakuwa sh. 5,000 wakati VIP A ni sh. 10,000.

Twiga
Stars ambayo kwa sasa haina mdhamini na kambini katika kambi ya Jeshi
la Kujenga Taifa (JKT) ya Ruvu mkoani Pwani kujiandaa kwa mechi ya
mashindano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Ethiopia.

Timu hizo zitapambana Mei 26 mwaka huu  jijini
Addis Ababa na kurudiana Juni 16 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam. Mshindi atashiriki fainali za AWC zitakazofanyika Novemba mwaka
huu nchini Equatorial Guinea.

No comments: