Social Icons

Wednesday, 23 May 2012

Redds Miss Chan'gombe hiyooo yaja!!

Mashindano
ya kuwania taji la Redds Miss Tanzania 2012 yanazidi kupamba moto kwa
ngazi za vitongoji nchini kote huku vitongoji kadhaa vikiwa tayari
vimesha fanya mashindano yake na vingine vikiendelea na maandalizi. 

Wakati
wiki hii Mashindano hayo yakitraji kufanyika katika Vitongoji vya
Kurasini Jijini Dar es Salaam tayari Wanyange wanaowania taji la Redds
Miss Cha'gombe 2012  nao wapo katika mazoezi tayari kwa fainali zao
zitakazo fanyika mapema mwezi ujao.

Pichani
ni warembo wa Chan'gombe wakiwa katika picha ya pamoja iliyopigwa muda
mfupi baada ya kumaliza mazoezi yao Mei 22,2012  katika ukumbi wa TCC
Chan'gombe jijini Dar es Salaam.
Warembo hao 11 wanataraji kupanda jukwaani mapema mwezi ujao kuwania taji hilo na kuwania tiketi ya kushiriki Miss Temeke 2012. 

No comments: