Social Icons

Monday, 28 May 2012

Rwanda yashutumiwa kuchochea uasi DRC


Umoja wa Mataifa umesema uasi ulioko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo unachochewa na nchi jirani ya Rwanda.
Taarifa ya ndani ya umoja huo ambayo BBC imeiona, inaishutumu Rwanda kwa kuwapatia silaha na askari waasi wa Congo.
Taarifa hiyo imezingatia mahojiano na waasi ambao wanasema waliandikishwa Rwanda kwa kisingizio cha kujiunga na jeshi la nchi hiyo, lakini walipewa silaha na mafunzo na kuvuka mpaka kwenda kupigana Congo.
Taarifa hiyo inasema mmoja wa waasi ni wa cheo cha chini.
Uasi huo, ambao ni wa hivi karibuni katika eneo hilo lenye mgogoro, ulianza mwezi Aprili baada ya baadhi ya maafisa wa jeshi la Congo kuasi.

No comments: