Jeshi la Uganda limesema kuwa limemkamata kamanda wa ngazi ya juu wa kundi la wanamgambo waasi wanaoongozwa na mbabe wa vita Joseph Kony la Lord’s Resistance Army LRA.
Kamanda ametajwa kuwa ni Caesar Achellam (Pichani) ambapo wachunguzi wa mambo nchini Uganda wamesema Achellam alikuwa sehemu ya uongozi wa juu wa kundi hilo linaloongozwa na Kony kuanzia miaka ambayo kundi hilo la LRA lilikuwa likifanya shughuli zake kaskazini mwa Uganda.
Kundi la LRA lilianza shughuli zake dhidi ya serikali ya Uganda katika miaka ya 1980.
Kiongozi wa kundi hilo Bw. Kony anatafutwa kwa madai ya uhalifu dhidi ya binadamu.
No comments:
Post a Comment