Na Mwandishi Wetu
HABARI hii haina lengo la kumhukumu mtu, mwenye uwezo huo ni Mwenyezi Mungu pekee, lakini Ijumaa Wikienda lina orodha ndefu ya warembo waliowahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na marehemu Steven Kanumba ‘The Great’ ambapo uchunguzi umethibitisha kuwa, kifo cha staa huyo kimewaacha ‘wajane’ hao katika vilio vya kila kukicha.
Uchunguzi makini uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa nyota huyo alikuwa na uhusiano na wasichana mbalimbali wakiwemo ma-miss, wanamuziki, wasanii wa sinema na wasio na fani yoyote ile.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha uhakika, kifo cha Kanumba bado kinawachuruzisha machozi wasichana hao kama inavyokuwa kwa wanawake walioolewa halafu wakaondokewa na waume zao (wajane).
‘Wajane’ hao waliotajwa kuendelea kumwaga machozi ni kama ifuatavyo;
WEMA SEPETU
Ni Mrembo wa Tanzania mwaka 2006/07 ambaye kwa sasa ni staa mkubwa wa filamu za Kibongo. Awali yeye na marehemu Kanumba walijaribu kuficha penzi lao lakini kadiri siku zilivyosonga, hakukuwa na kificho tena.
Kifo cha Kanumba ni pigo kwake, bado anamlilia hadi sasa. Wakati wa msiba alikiri kuwa hakuwahi kutengana moja kwa moja na marehemu.
SYLVIA SHALLY
Ni mrembo wa Miss Dar City Centre 2009, alikuwa na uhusiano na Kanumba, walianza walipokutana katika shindano la kumtafuta Unique Model kwenye Hoteli ya Giraffe, Dar.
Yeye bado hajaamini kama staa huyo aliaga dunia ghafla.
QUEEN SUZY
Ni Mnenguaji wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, aliwahi kudaiwa kuwa na uhusiano na marehemu Kanumba wakati fulani akipiga mzigo kwenye Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta International’ ambapo mara nyingi Kanumba alikuwa akienda nyumbani kwake.
Anasema kifo cha Kanumba mpaka sasa bado ni ndoto kwake na hakuamini.
Habari kwa hisani ya GPL

No comments:
Post a Comment