Social Icons

Tuesday, 31 July 2012

Hii Iwafikie vijana wote wakiume:Ukishanunua suti ‘suit’ yako ondoa vile vibandiko ‘tags’ kutoka kwenye mkono wa suti ya ‘sleeve’. Hasaa mkono wa kushoto.


 
Hii wasome wanaume tu: Ukishanunua suti ‘suit’ yako ondoa vile vibandiko ‘tags’ kutoka kwenye mkono wa suti ya ‘sleeve’. Hasaa mkono wa kushoto.

Kuna mazoea ambayo naona siku hizi yamejengeka kwa wanaume na vijana watanashati, kuvaa suti ‘suit’ bila ya kuondoa vibandiko ‘tags’, jambo hili linafedhehesha mno.

Watu wamekuwa wakivaa suti zao bila ya kuondoa hivyo vibandiko ‘tags’, wakifikiri kuwa ni sehemu ya nguo kumbe hapana.

Kuna watu kadhaa niliowauliza kwa nini wamekuwa wakivaa suti zao na kuacha hivyo vibandiko, jibu lilikuwa huzivaa wakidhani ni sehemu ya nguo na wengine walisema ni kwa ajili ya ufahari ‘show off’ kuwaonyesha watu wengine aina za suti zenye majina.

Ujumbe wangu ni mmoja tu kwa wavaa suti, muwe mnaondoa hivi vibandiko kutoka kweye mikono ya suti zenu mara baada ya kununua. Inawezekana wengi hawafahamu kuwa hivi vibandiko ‘tags’ ni kwa sababu ya matangazo ya kibiashara, kutangaza aina ya suti, majina ya wabunifu na kampuni ziliyotengeneza suti hizo, na zinaweka ili mnunuzi hata akiwa mbali aweze kutambua mambo hayo niliyoorodhesha hapo juu na si vinginevyo.

Wito wangu kwako ambaye ulikuwa haufahamu kuwa kuvaa vibandiko ‘tags’ si kitu kizuri na kinafedhehesha, uwe unaziondoa mara tu unaponunua suti yako. Unaweza kuziondoa kwa kutumia mkasi mdogo, wembe au kuna kifaa maalum kwa ajili ya kazi hiyo.

No comments: