Social Icons

Monday, 9 July 2012

Siku moja moja baada ya Libeneke huwa nakatiza mitaa!



 Hapa Nilikuwa nangoja Gogo lipite ili nipande niendelee na mambo yangu
 Hili Ni bonge la Posta ambalo lipo mitaa ya kati
 Ni Baadhi ya maeneo 
 Hapa nikiwa na mtu mzima Jerry ambaye amekaa kulia kwangu baada ya kujenga mwili 
Hapa nipo kati kati ya mtaa Flan nikijaribu kupata ukodaki kama kawa ...

Siku zote baada ya kuwaletea habari kibao na kuwafahamisha nini kinaendelea duniani Basi nami hupata kamuda japo kidogo kutazama huko nje kunaendelea nini, Hapa ilikuwa ni siku ya Jumamosi kuamkia jumapili ambapo nilikuwa nimetoka zangu maeneo mbali mbali kunyoosha miguu na baadae kurudi zangu maskani kuendeleaza Libeneke kama kawa. Ndio maana siku kama Jumamosi na Jumapili mara nyingi huwa nazunguka tu... Pamoja sana wadau na asanteni kutembelea Libeneke hili..

No comments: