Social Icons

Wednesday, 15 August 2012

Exclusive One: Hivi ndivyo nilivyo Malizia Mambo yangu ya Nondo'z na Kukabidhi pepa langu ...... Namshukuru Mungu kwa yote

 Hapa nilikuwa zangu  kituo cha Treni za mwendo kasi Nikingojea kuondoka kwenda kupeleka  pepa zangu za Nondoz.. Kama kawa naendelea kublogisha.
 Hapa nimeingia ndani ya Gogo 
Baada ya kufika tuu nilafungua mavitabu yangu ma nne ambayo yalikuwa ni mazito balaa
Haya ndio mavitabu yangu ambayo yamefanikisha mimi kumaliza Nondoz

 Nilipata muda wa kuperuzi kwa mara ya mwisho kabla sijaenda ku submit rasmi
 Daaah hapa ninafuraha ajabu maana daah mambo ya shule ndio bye bye 
 Sikuwa na amini amini kama ningeweza kufikia hatua ya kula Nondoz, Lakini hapa ndipo ilikuwa dakika 5 kabla ya mimi kuwakiliza pepa zangu.

 Baaada ya  kuwakilisha pepa zangu nilipata ukodaki wa nguvu ndani ya Bango kubwa la skuli yangu , Kama inavyo someka hapo, Chuo cha ukweli ambacho ni full Technology no Analogy hapa
Hapa nimesha maliza kuwakilisha pepa langu, Mambo yote yamepita sawa sawa sasa ukafika muda wa good time, nikaamua kwenda jichanganya zangu na watalii wengine kibao...

***********
Na Fredy Tony Njeje
Kwa hakika Jana ilikuwa ni siku yangu ya Pekee sana ambapo kwanza kabisa kabla sijaenda mbali sana napenda sana kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha safari yangu ndefu sana ya kielimu kuanzia Darasa la vidudu mpaka kufikia hapa nilipo fikia mwisho kabisa wa Elimu naweza sema hivyo kwa maana kwenda kufanya PhD ni kwa wale wanaotaka kuwa watafiti na wanaohitaji kufundisha, Nasema mwisho kwa sababu ndio mwisho wa kufanya mitihani na kupigishana kelele na walimu, Naongeza kusema mwisho kwa sababu levo hii mtu unaweza kufanya ishu yoyote ikiwa ni pamoja na kufundisha vyuo vikuu na mambo mengine mengi.

Pili napenda sana kuchukua nafasi hii kumshukuru msimamizi wangu ambaye ndiye aamefanikisha mpaka safari yangu ipate fanikiwa.

Hii sio ya Tatu, Lakini kipekee kabisa napenda kuchukua nafasi hii kushukuru familia yangu kwa ujumla akiwemo Marehemu Baba yangu ambaye ndiye niliye mdedicate katika kazi yangu.. pia napenda kumshukuru Mama yangu, Kaka yangu na dada yangu kwa kunipa sapoti kubwa sana katika kufanikisha mambo yangu ya shule.

Tatu napenda kuwashukuru ndugu jamaa na Marafiki kwa kunisaidia kimawazo, kimali na mambo yote sito weza mtaja mmoja mmoja lakini Mungu awabariki sana awazidishie zaidi na zaidi.

Mwisho napenda kusema kwamba katika Elimu Graduation ni kielelezo tuu cha kufurahi,hasa katika elimu za level zote, lakini kumaliza na kuwa na Pepa lako hapo ndipo mwisho wa kila kitu. na si lazima kuhudhuria hata hiyo Graduation.. 

Aluta Kontinua Mapambano yanaendelea

Asanteni sana,
Fredy Tony Njeje
Mkurugenzi Mtendaji wa Blog hii
Head of Group Research and product development- Tone Multimedia Company Limited
General Secretary- SEDI NGO 
Director of IT and Online Tourism Promotion-Miss Tourism Organisation

No comments: