Social Icons

Tuesday 28 August 2012

Hii Imetokea Tanzania: Jaribio la kutaka kumlawiti mtoto: Akung'utwa hadi kuachiwa Daktari na Mungu wamponye



 Sura ya mtoto imefichwa kutokana na maadili
Huyu ni mtoto Jina Limehifadhiwa mwenye umri wa
miaka 8, alikuwa nyumbani wakati wazazi wake wote wakiwa hawapo, Alikuwa
yeye na kaka yake mwenye umri wa miaka 12.Ndipo swahibu lilipomkuta mpaka kufanya aumizwe kiasi hiki


 Huyu ndio mtuhumiwa baada ya kupata kipigo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasiri
Mtuhumiwa akipandishwa kwenye gari la polisi
---
Alifika nyumbani na kumlaghai mtoto Jina Limehifadhiwa kwa pipi na kumuita uncle, uncle.

Akamvuta mpaka vichakani.

Akiwa tayari ameshashusha nguo, akataka kumlawiti.Mtoto alipoona hivyo akaanza kupiga kelele na kupambana na mtuhumiwa.

Mtuhumiwa
wa uasi alipoona mtoto anapiga kelele, akaanza kumshambuliwa kwa
kumng'ata kwa meno mashavuni na kisha kumpiga na jiwe kwenye paji la
uso.

Kwa bahati nzuri, mama aliyekuwa anashusha matofali jirani
alisikia purukushani za kelele hizo kabla ya tendo baya la ulawiti
kufanyika. Ndipo mama yule akawaita watu ambao walimkuta mtuhumiwa akiwa
anaendelea na jaribio lake hilo la kulawiti.

Mtuhumiwa
alifanikiwa kumwaga haja zake, ila hakufanikiwa kumuingilia mtoto
kimwili, ndipo watu wenye hasira walipompa adhabu yake na yeye, kabla
Polisi kufika na kumtia mbaroni.

Inasemekana kuwa mtuhumiwa huyu
ndiyo tabia yake, mitaa ya Mbezi ya Kimara, amezunguka sana kuharibu
watoto wa watu, ila hii ndio ilikuwa arobaini yake. Kila Nyumba akifika
anauliza baba na mama wapo? akijibiwaa hawap,o anaanza shughuli zake.

Hivi sasa yuko mahututi katika Hospitali ya TUMBI, akingojea kusomewa mashtaka.


*Ukitaka kufwatilia kwa ukaribu uodate nzima ju ya tukio hili la kusikitisha endelea kulifwatilia kupitia LadyJayDee blog 

No comments: