Social Icons

Tuesday, 30 October 2012

BLOG YA FREDY TONY NJEJE YATIMIZA MWAKA MMOJA.



©Fredy Njeje






Hivi ndivyo nilivyo anza Safari yangu ya kublogisha  Tar 30.10. 2011, katika post hiyo ya juu nilitengeneza slide show hiyo ikiwa ni moja ya pongezi zangu kwa Blog ya Jamii ya Issa Michuzi. na ndiyo ilikuwa post ya kwanza kabisa kwa Libeneke hili, Siku hiyo kama inavyo onesha hapo hakuna mtu hata mmoja aliye tembelea yani 0, sikufa moyo mambo yaliendelea mpaka leo hii natimiza Mwaka mmoja.

***************
Kwanza kabisa napenda kumshukuru sana Mungu mwenyezi aliyenipa nguvu na afya njema pasipo kusahau kipawa ambacho  hakika naendelea kukidumisha.

Leo Blog yangu changa kabisa inatimiza mwaka mmoja. Napenda moja kwa moja kuwashukuru kama ifuatavyo.

Kwanza kabisa Shukurani zangu za dhati kabisa ziwafikie wadau wangu na wasomaji wakubwa wa blog hii ambapo bila nyie hapo mimi nisingekuwa na nguvu ya kufanya hii kazi ya kuwapa habari mbalimbali, maana tofauti na Blogs zengine blog hii imejikita zaidi katika maisha halisi na mambo yanayo tokea katika jamii yetu, Hakuna maswala ya Siasa humu. Kwa misingi hiyo napenda kuwasihi  Muendelee kutembelea siku hadi siku.

Kipekee kabisa napenda kutoa Shukurani zangu kwa Bloggers wenzangu wote ambao kwa njia moja au nyengine tumekuwa tukishirikiana sana katika kazi na mambo mbali mbali, Nitapenda ku wataja baadhi ambao tumekuwa tukifanya kazi pamoja hata kabla sijafungua blog hii

Rama S. Msangi, Joseph Lukaza, Cathert Angelo, Ahmad Michuzi, Issa Michuzi, Othman Michuzi, M. Mjengwa, Jestina George, Sarah Peter, Simon Kitururu, Dj Choka, Faith Sabrina Hilary, Joseph Mwaisango, Mubelwa Bandio, Mroki T. Mroki, Evarist Chahali, Francis Godwin, Mahamila Rajab, King Kif, Abby Mrisho, Haki Ngowi, Greyson Salufu, John Kaindika  pamoja na wengine kama sikuwataja katika Group hili ni kupitiwa tuu lakini Tambua kuwa Jina Lako Lipo hapo, Hawa ni wale ambao Nimefanya nao kazi kuanzia mwaka 2010 mpaka sasa bado tupo pamoja katika kila Jambo Mimi naweza sema ndio walio nifanya niendelee kubaki katika Game.

Katika safari yangu nimekutana na Malicky Boaz, Salim Chuma, Hussein Rashid, Fununu Habari, Maidiana, Fanuel, Tina Ndonde , Megvictor Mash, Gregory Kadendula, Brizzleo Blogspot, Abuu, Jacque Wilbard , Joyce Mahila, Eddie,  Ester Ulaya .. Hawa ni marafiki wapya kabisa katika Kublogisha pia napenda kuwashukuru sana kwa Mchango menu mkubwa wa kimawazo na mambo mengine mengi mengi

Hii ni Safari tuu na inaendelea , nina waahidi mambo mengine makubwa zaidi, kama mlivyo ona mwaka mmoja ulio pita nilianza na watu 0 sasa nina watu zaidi ya 300,000+

Mpaka naandika hapa hii chini ndio idadi yawalio tembelea
313,816
Fredy Tony Njeje
Asanteni sana
Imetolewa na Msimamizi wa Blog Hii
Fredy Tony Njeje



No comments: