Social Icons

Tuesday, 30 October 2012

MAKUBWA HAYA: RAIA MMOJA WA BRAZILI AZUA UTATA BAADA YA KUHUDHURIA KATIKA MAZISHI YAKE.




Familia moja nchini Brazil ilikumbwa na kizazaa baada ya ndugu yao kuwasili wakati familia hiyo ikifanya mazishi yake.
Mazishi ya Bw. Gilberto Araujo (pichani kulia) mwenye umri wa miaka 41 anayefanya kazi ya kuosha magari yalikuwa yakifanyika katika mji wa Alagoinhas wakati alipojitokeza.
Sakata hilo lilitokea baada ya kaka yake Jose Marcos kuutambua mwili mmoja katika Nyumba ya kuifadhia maiti na kusema ni mdogo wake na ulichukuliwa na kupekwa nyumbani kwa mama yao kwa mazishi.
Araujo alichukua hatua ya kukimbilia nyumbani kwa mama yao baada kukutana na rafiki yake mtaani ndipo alipoambiwa nyumbani kwenu kuna msiba wanafanya mazishi.
Inspekta wa Polisi Roberto Lima amesema ilimbidi awahi kwa ili kuwataarifu ndugu na jamaa zake kuwa yu mzima wa afya.
Inaelezwa kuwa baadhi ya watu walizimia na wengine walikimbia vibaya sana baada araujo kuwasili msibani.
Shemeji yake Araujo amefahamisha kuwa mkanganyiko huo ulitokea baada ya taarifa kanza kuzagaa kuwa muosha magari huyo amepigwa risasi na kufa.
Hata hiyo ilikuja kubainika kuwa mwili ule ulikuwa ni mtu aliyejulikana kama Genivaldo Santos Gama ambaye naye pia ni muosha magari.

Mo Blog

No comments: