LICHA ya kuomba radhi kutokana na kuvaa nusu uchi katika matamasha ya Fiesta mwaka huu, wasanii wa filamu nchini, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wamesema wataendelea kuvaa nguo hizo.
Wakizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), jijini Dar es Salaam jana, wasanii hao walielezea kujutia tukio hilo ambalo hawakulitarajia kutokea.
Walisema wao kama wasanii wa filamu, wanalazimika kuvaa mavazi kulingana na wakati na tukio husika, ndiyo maana walivaa mavazi yale, lakini tatizo lilikuwa ni urefu wa jukwaa.
Mmoja ya wasanii hao, Aunt Ezekiel alisema kwamba kilichotokea ni bahati mbaya kwani hawana uzoefu na majukwaa ya muziki na matokeo yake kuwa hivyo.
“Yale mavazi huwa tunayavaa kila mara, lakini kwa bahati mbaya jukwaa lilikuwa refu na ndiyo maana tulionekana hivyo…tunaomba msamaha na tumeshajifunza.
Tunapenda kuchukua fursa hii kuiomba radhi jamii yote, ndugu jamaa na marafiki kwa tukio hili ambalo hatukulitarajia,” alisema Aunt Ezekiel.
Akizungumzia tabia yake ya kupiga picha za utupu, Aunt alikana na kudai kwamba; “Hizo picha wanazodai ni za utupu si kweli, bali nilipigwa mgongo kwa ajili ya jalada la filamu ya Young Millionea.
Hizo nguo fupi sijaanza kuvaa jana wala juzi, hivyo kwa tukio lile ilitokea bahati mbaya na kuanzia sasa nitakuwa makini na vitu kama hivyo,” alisema Aunt Ezekiel.
Naye Wema, pamoja nakuomba radhi aliitaka jamii kutowachukulia vibaya kutokana na mavazi hayo, kwani mara nyingi wanavaa kulingana na wakati na mahali.
Alisema baada ya dosari hizo kujitokeza, aliamua kuanza kuvaa suruali za jeans au kaptula ili kuepukana na kitendo hicho.
Kwa upande wake Katibu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Wilson Makubi alisema baada ya tukio la wasanii hao, waliwaita na kuzungumza nao na mwisho wa siku walikiri makosa na wakaomba radhi.
Chanzo:daiama
No comments:
Post a Comment