WAKATI ikidaiwa kuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya Matonya, alifungiwa ndani kimapenzi na mmoja ya wasanii wa bongo movie na kulizwa shilingi za kitanzania milioni 6, sasa ameamua kuweka wazi kuwa wanawake wa tasnia hiyo ni michosho kwani wanapemnda hela na wanaleta maigizo hadi kwenye mapenzi.
DarTalk ilimtafuta Tonya Boy na kuzungumza naye juu ya ishu hiyo kuwa kulikoni hadi alilizwa kiasi hicho cha pesa, ndipo alipodai kuwa kuna mmoja wa mademu wazuri wanaovuma kwenye tasnia bongo movie ndiye aliyefanya mchezo huo mchafu kwani alijifanya anampenda sana kumbe alikuwa anamuigizia na alikuwa na ishu yake.
Alidai kuwa baada ya tukio hilo kutokeo demu huyo hakumuona tena na alikuja kusikia yupo mkoani kitu ambacho kilimfanya aishiwe nguvu kwani hakuamini kilichotokea na hapo ndipo alipoamini kuwa mademu wa tasnia hiyo ni wapigaji na ukiwaonesha kwako utajuta.
“Bongo movie hakuna demu yani hata bure siwataki tena yani wanaleta maigizo hadi kwenye mapenzi dah kweli hii tasnia ina laana na inahitaji kuombewa kwani wasanii wake wanatamaa ya hela na wanamapepo ya ngono yani wakimuona mwanaume ana hela basi mate yanawatoka, hata wa bure siwataki tena,” alidai.
Hata hivyo alipoulizwa jina la msanii huyo wa filamu alishindwa kumtaja kwa madai kuwa hata kama aliiba kiasi hicho cha pesa lakini kwa upande wake hana bifu naye ingawa hatamani hata kumuona.
No comments:
Post a Comment