Kwa muda mrefu matajiri wengi walitamani kulinunua jumba la kifahari la marehemu Michael Jackson ambalo pia linakumbukumbu kubwa kwa kuwa ndipo alipofia mfalme huyo wa Pop, sasa jumba hilo limepata mnunuzi na limeshalipiwa mkwanja wote unaostahili.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ jumba hilo limenunuliwa na Steven Mayer ambae ni tajiri mkubwa na muwekezaji katika masuala ya bank.
Vyanzo mbalimbali vinaonesha kuwa jumba hilo limeuzwa kati ya dola za kimarekani million 17 na dola million 20, na lilikuwa limepangwa kuuzwa karibia dola za marekani million 24, ambazo zikibadilishwa kwa shilingi za kitanzania yatakuwa mabilioni kibao.
Inaonesha kuwa mnunuzi huyo anahamu kubwa ya kuingia katika jumba hilo kiasi kwamba amehamia wiki moja kabla ya umiliki wa mtu aliyekabidhiwa kuiangalia haujafungwa rasmi.
Kinachofurahisha zaidi ni kwamba muuzaji nae amemruhusu Mayer ahamie kwenye jumba hilo hata kabla hajasitishiwa rasmi umiliki ama uangalizi wa jumba hilo la kifahari, japokuwa anasitasita kwa kuwa anaona ni risk kwake.
Steven Mayer anaonekana analipenda sana jumba hilo kati ya matajiri wengi ambao walikuwa wanalitamani jumba hilo kwa hiyo kwa bei yoyote alikuwa tayari kulinunua na kushare baraka za Michael Jackson kwenye mjengo huo.
Imeandikwa na Leo Tainment
No comments:
Post a Comment