Social Icons

Wednesday 31 October 2012

SUMA LEE AIBIWA GARI




Kama utakuwa na kumbukumbu nzuri haina shaka kuwa utakuwa unakumbuka stori iliyochukua nafasi kwenye kipindi cha XXL siku chache zilizopita juu ya nyota wa songi la 'Hakunaga' Suma Lee kupata ajali wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Kigoma kwa ajili ya kupiga shoo.
Taarifa kutoka Coco Beach zinasomeka kuwa nyota huyo mzaliwa wa mkoa wa Tanga ameibiwa ndinga yake hiyo aina ya Land Cruiser VX mwishoni mwa wiki iliyopita wakati alipokuwa kwenye mapumziko ya wikiend katika ufukwe wa bahari ya hindi.
haikuwa siku nzuri kwangu, nimeibiwa gari na watu ambaoa nahisi walikuwa wanaifuatilia kwa siku nyingi maana hata wakati wanaiba watu walikuwa karibu waliniambia kuwa watu hao hawakuvunja wala mkuharibu chochote walichokifanya ni kufungua mlango kama ambavyo mimi huwa nafanya na kuwasha gari kisha kuondoka


No comments: