Social Icons

Tuesday 13 November 2012

HATARI: MKE AMFANYIA UKATILI MKUBWA MUMEWE . SHUHUDIA


KIZITO Mahamba (50) (pichani), mkazi wa Mwananyamala Mtaa wa Msili B jijini Dar es Salaam, amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala wodi namba 5A baada ya kufanyiwa ukatili wa kutisha na mkewe ambaye amemmwagia maji ya moto mwilini.
Akizungumza na gazeti hili huku akiwa katika hali mbaya wodini alikolazwa, Mahamba alidai kuwa mkewe, Rabina Mkakamba (38) kabla ya kufanya tukio hilo alianza kuonyesha dalili za kumdharau kila alipojerea nyumbani.
Siku ya tukio ambayo ilikuwa Oktoba 20, mwaka huu, mke wangu hakuwa katika hali ya kawaida maana kila nilichomwagiza kufanya alikataa, nikajiuliza kulikuwa na nini?
“Hayo yote yalipokuwa yakiendelea,  jikoni alikuwa anachemsha maji, nikiwa nimelala nilishitukia  mke wangu akiingia chumbani na chupa ya chai ambayo alinitupia na maji kuniunguza sehemu kubwa ya mwili wangu, nadhani alitaka kuniunguza usoni. Baada ya kufanya kitendo hicho alichukua sanduku la nguo zake na fedha zangu na kutoweka huku akiniacha nikigaagaa .
“Nililetwa hapa hospitali na mtoto wa ndugu yangu na ndiye anayenisaidia,”  alisema Mahamba.
Gazeti hili lilimtafuta mama  Rabina na alipoulizwa kama alifanya kitendo hicho, alikiri na kuongeza kuwa anampa pole mumewe na pedha alizochukua aliahidi kumtumia  kwa njia ya Tigo Pesa ili zimsaidie kujiuguza
chanzo:globalpublishers

No comments: