Social Icons

Wednesday, 12 December 2012

MAMA KANUMBA AMBARIKI MRITHI WA MWANAYEMAMA wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa ametoa baraka zake kwa mwigizaji chipukizi, Philemon Lutwaza ‘Uncle D’ ambaye anatarajia kuigiza katika filamu ya After Death ambayo ni maalum kwa kumuenzi marehemu mwanaye, Imelda Mtema anashuka nayo.
Akizungumza na paparazi wetu juzikati, mama Kanumba ameweka plain kuwa ameridhishwa na uwezo wa Uncle D na anaimani kuwa ataweza kuziba pengo la marehemu katika nafasi ya kucheza na watoto wale aliokuwa akiigiza nao marehemu
Namshukuru sana Jacqueline Wolper kwa kuandaa filamu ya After Death maalum kwa ajili ya kumuenzi mwanangu. Nina imani kila kitu kitakwenda vizuri na mimi nimewapa baraka zote ,” alisema mama huyo.
chanzo:globalpublishers

No comments: