Kila mtu anaweza akawa anamiliki mtandao wake wa kijamii hasa Blogs..... lakini katika hizo mamia za blogs zilizopo hapa Nchini wengi tumekuwa sio wabunifu...
Kwa nini labda sio wabunifu?.... Hii ni kutokana na kwamba watu wamekuwa wakidhania kwamba kuendesha mtandao ni kutupia tu Bora Story....
Sawa kuna watu wanatembelewa mpaka na wadau 50,000 kwa siku.... lakini umesha wahi tembelea mitandao yao ukaona wanaweka nini hapo?.... Jiulize kwanza.
Leo hii katika pita pita zangu za mitandao mingi sana nimekutana na Moja ya Blog za Mtanzania mwenzetu inayo kwenda kwa Jina la MWANADADA kimsingi blog hii nimekuwa nikiifuatilia kwa muda mrefu sana lakini hata hivyo nimekutana na mambo mengi sana ambayo kimsingi yapo tofauti sana na blogs zengine ....
Ukitazama Home page yake kwanza utapata picha kamili ya Blog yake inahusiana na nini kama inavyo onekana hapo, kwamba alicho kiandika hapo ndicho anacho kimaanisha ... na si vinginevyo kama mtu mwengime mfano anasema HII NI BLOG YA BURUDANI... lakini ukiingia humo ndani unakutana na kila kitu ambavyo sasa havihusiani hata na maudhui ya Blog hiyo.
Blog Hii ya mwanadada imekuwa na mpangilio kama vipindi vya Radio ama Televisio... kwa nini?
Hii ni kwa mfano hii safu ya Mtoko Ideas imekuwepo Tangu muda na huwa ni Post za muendelezo... mfano huu hai huwafanya watu wengi wavutike na kuja kutazama nini Blog ya MWANADADA imeweka... na kusababisha kuwe na watu maalum ambao hawawezi kulala bila kutazama safu hii....
Kuna kipande cha Maneno mbalimbali ambayo yapo na yanaujumbe mzito... kipande hiki pia kimekuwa ni kivutio cha watu wengi hasa watembeleaji wa mtandao wake.......!
Pia zaidi ya hapo Blog hii inakupa nafasi mbalimbali kama inavyo onekana hapo juu...!
Kwa kumalizia tuu ni kwamba ..... Mwanadada Blog imeonesha utofauti mkubwa sana .. kwa sababu yeye anajua anacho kifanya.... anajua watu gani wanatakiwa afanye nini.....
Mwisho... napenda kumpa pongezi nyingi sana .....
Mtembelee sasa katika Blog yake Bofya hapa MWANADADA BLOG
Like Facebook Page yake Bofya Hapa MWANADADA
Bofya hapa ku Follow Twitter yake: MWANADADA
Stay Tuned Kwa Blogger wetu atakaye Fuatia ....
Good Bye!




No comments:
Post a Comment