Ilikuwa ni Simanzi kubwa siku ambayo tulipatwa taarifa ya kushtushwa kuwa Ndugu yetu na jamaa yetu Mpendwa Ritha ametutoka....
Japo Taarifa ile ilikuwa ni ngumu kuamini lakini ukweli ukabaki kuwa ni kweli alikuwa amefariki Dunia....
Marehemu Alianza kusumbuliwa na kuumwa mnamo mwezi wa kwanza kwa tatizo la ini mpaka mauti ilipo mfikia tarehe 3.11.2013 ..
Kiukweli Mume wa Marehemu Bwana Gregory Mwanyika Binafsi nina mfahamu sana na hata alipo pata taarifa hizi za msiba alishindwa kuamini hadi siku ya tarehe 5.11.2013 alipo mwagia kaburini mchanga kwa mara ya mwisho...
Hivi ndivyo Safari yake ya mwisho ilivyo kuwa....

Marehemu Ritha enzi za uhai wake
Waombolezaji Mbalimbali wakiwa Msibani Kimara Stop over
Rafiki wa Marehemu wakiwa wanawasili Msibani
Mwili wa Marehemu ukiwa unawasili Nyumbani
Mchungaji akiwa anasali na kutoa neno wakati wa ibada hiyo ya Mazishi nyumbani
Waombolezaji wakiwa ndani
Waombolezaji Ndugu jamaa na marafiki wakiwa wanasikiliza kwa umakini
Mume wa Marehemu Bwana Gregory Mwanyika akiwa katika Majonzi makubwa
Wa kwanza kutoka kulia aliye kaaa ni Masache kasaka mmoja wa marafiki wakubwa wa marehemu akiwa na waombolezaji
Jeneza la Marehemu Ritha
Waombolezaji wakati wa ibada ya mazishi
Msemaji wa Familia akitoa Maelekezo
Msemaji wa Familia akitoa wasifu wa Marehemu
Shukurani zikitolewa
Bwana Gregory Mwanyika Mume wa Marehemu Ritha aliye vaa shati jeusi akiwa katika mawazo na simanzi
Mume wa Marehemu Bwana Gregory Mwanyika , akitoa Heshima za mwisho
Bwana Masache kasaka akitoa salam za mwisho
Baba wa Marehemu Ritha akitoa heshima za Mwisho kwa uchungu , huku akiwa amemshika Marehemu kwa Mara ya mwisho
Mama wa Marehemu aliye vaa Nguo nyeupe akitoa Heshima za mwisho
Dada wa Marehemu akitoa Heshima za Mwisho
Mtoto wa Marehemu akitoa heshima za Mwisho
Mchungaji alitoa Heshima za Mwisho
Mume wa Marehemu Bwana Gregory Mwanyika akiwa katika Gari Maalum lililobeba Mwili wa Marehemu
Safari ya Kuelekea makaburini maeneo ya kibanda cha mkaa
Mume wa Marehemu wa kwanza kushoto Bwana Gregory Mwanyika akiwa katika shughuli ya maziko
Waombolezaji
Safari ya mwisho inaelekea ukingoni
Mchungaji akiliombea kaburi kabla ya kuzika
Mwili wa Marehemu unaingizwa Kaburini
Mwili wa Marehemu ukiwa kaburini
Mtoto wa marehemu
Mume wa Marehemu Bwana Gregory Mwanyika akiweka mchanga katika kaburi kabla ya kuanza kufukia
Kazi ya kufukia kaburi inaanza
Mume wa Marehemu Bwana Gregory Mwanyika akiweka taji la maua katika kaburi la Mke wake
Wazazi wa Marehemu wakiweka Shada la Maua
Dada wa marehemu akiweka shada la maua
Mume wa Marehemu Bwana Gregory Mwanyika akiwasha mshumaa
Marafiki wakubwa wa Bwana Gregory Mwanyika kutoka kulia ni Fredy Tony, Winfred Mbwilo na Masache Kasaka ...
Mume wa Marehemu Bwana Gregory Mwanyika akiwa na mwanae kaburini baada ya maziko
Marafiki wa kubwa wa Marehemu na ambao alisoma nao zamani Mbalizi Sekondari huko mkoani Mbeya kutoka kushoto ni Fredy Tony, Masache Kasaka, Winfred Mbwilo na Elina Hongoli
Tumerejea Nyumbani baada ya msiba...
Kwa Niaba ya wote ... na Blog hii tunawapa pole sana wafiwa Mungu azidi kuwapa nguvu hasa Mume wa Marehemu Bwana Gregory Mwanyika .
Imeandaliwa na kupigwa picha na Fredy Tony rafiki mkubwa wa Mume wa marehemu bwna Gregory Mwanyika.
BWANA AMETOA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
AMEN
No comments:
Post a Comment