Hakika hii ilikuwa ni safari ndefu sana ambayo ilikuwa na mabonde na maporomoko kibao... lakini kwa uwezo wa Mungu muumba siku ya tarehe 13.12.2013 safari hii ilifikia mwisho pale ambapo mdau wetu wa nguvu Tabitha Hudson alipo Kamata fursa yake ya kumaliza rasmi chuo, ni katika chuo cha uandishi wa Habari cha DSJ....
Kimsingi kila mtu anafahamu kuwa elimu ndio ufunguo wa maisha na ndio maana tunakomaa madarasani kupiga shule ....
Sasa mdau wetu ndio amesha malizana na maswala ya chuo na sasa yupo kamili kabisa kujenga Taifa kwa kutumia karamu yake...
Tutazame kwanza safari yake ilikuwaje...
Mdau Tabitha hapa akiwa na mazawadi kibao ambayo alipokea kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki .
"Hakika namshukuru Mwenyezi Mungu sana kwa kuniwezesha kufika mpaka hapa nilipofikia ... " Aliyaongea haya moyoni wakati akitoa Mkono wa Asante kwa Mgeni rasmi Mkuu wa Chuo na wengine waliofika katika mahafali hayo. 
Mdau Tabitha hapa aikiwa anangojea mahafali yake kuanza
Mdau Tabitha akiwa na Baadhi ya marafiki zake wakati wa mahafali hayo
Mdau Tabitha wa kwanza kutoka kulia mstari wa pili akifuatilia kwa umakini mahafali
Ilikuwa ni mwendo wa furaha tuu
Kila mtu na lake hapa
Mahafali yakiwa yanaendelea
Kutoka kushoto ni Mama mdogo wa Tabitha akiwa na Tabitha katikati pamoja na Rafiki yake.
Ni kupendeza tuu
Tabitha akiwa na mdogo wake
Hapa Wakiwa wanacheza kwaito Mara baada ya mahafali
Hii ndiyo ile Keki aliyo itafuna Tabitha wakati wa mahafali yake.... msomaji tulikula kwa niaba yako...
Baada ya kutaza tukio zima ......
Kwa niaba ya wasomaji wangu wa ukweli sana ..... Naungana nanyi kwa pamoja kumpongeza sana mdau Tabitha kwa mahafali yake ... ambapo yalikuwa ni ya 19 katika chuo cha uandishi wa habari cha DSJ.
No comments:
Post a Comment