Social Icons

Saturday, 14 December 2013

HONGERA SANA ZOURHA KWA KUMALIZA CHUO..

Siku zote mtu anapofanikiwa katika jambo huwa na furaha hiyo ikiwa ni alama ya ushindi mkubwa, maana katika safari siku zote wapo ambao watashindwa mwanzoni, wapo ambao watafika mpaka nusu, wapo ambao watakata tamaa na wasiweze fika na wapo ambao watamaliza safari yao kabisa...
Tarehe 13.12.2013 ilikuwa ni moja ya tarehe muhimu sana kwa mtu wetu wa ukweli sana Zourha pale alipohitimu mafunzo yake katika Chuo cha uandishi wa habari cha DSJ ikiwa mahafali yake ni ya 19 katika chuo hicho.. Kwa hakika yeye aliweza kumaliza salama safari yake na kuungana na wenzake katika sherehe hizo zilizofanyika katika viwanja vya Msimbazi Centre .
Na hivi ndivyo ilivyokuwa
 Mdau wangu Zourha wa mbele akitoa mkono wa asante kwa mgeni Rasmi, Mkuu wa chuo cha uandishi wa habari -DSJ pamoja na viongozi mbalimbali waliofika katika mahafali hayo ya 19 katika chuo hicho
 Wakiwa wamependeza wahitimu huku Zourha wa pili kutoa kulia aki show Love na rafiki zake ..
 Chukua Pozi pata Ukodaki wa Nguvu hapa....
 Zourha wa pili kutoka kulia akiwa anacheza muziki ni wakati wa mahafali ya chuo hicho cha DSJ
 Hapa kila mtu yupo na furaha
Nikipata ukodaki wa nguvu na Zourha 

Mwisho napenda kuchukua nafasi hii kukupongeza sana kwa hatua kubwa uliyofikia mpaka sasa.... Pia kwa niaba ya wasomaji wote wa kona hii sote yani tunakupa hongera mingi mingi 


No comments: