Siku zote unapo hesabu Miaka huwa hairudi nyuma lakini huenda mbele.. Haingoji labda itasimama kwanza umalize mambo yako ndio iendelee kusonga mbele...
Hivyo hivyo hata sisi wanadamu hata siku moja tangia tunakuja Duniani mpaka tunaendelea kukuwa hukuwa kulingana na miaka inavyo sogea mbele...
Leo ni siku , mimi naweza kusema ni siku maalum kwa Rafiki yangu Neema ambapo leo hii anakumbuka siku yake ya Kuzaliwa, ikiwa anatimiza Miaka kadhaa ambayo nauhakika itakuwa nimiaka mingi ambayo pia yenye malengo yake ndani yake, Nikupe Hongera sana kwa Mwaka uliopita ya kwamba ulitimiza Malengo yako mengi ikiwa ni Pamoja na Kupata Shahada yako ya pili.Basi katika Mwaka huu ambao ni mwaka mpya kwako, nakuombea uwe mwaka wa Mafanikio zaidi, Upate kutimiza yale yote uliyo yapanga.
Mwisho nikutakie Afya njema...
Happy Birthday

No comments:
Post a Comment