Social Icons

Tuesday, 7 October 2014

NIKIWA MZUZU NCHINI MALAWI HII ILIKUWA DINA YA NGUVU TULIYO ANDALIWA NA WENYEJI WETU.

Hii ilikuwa ni moja ya Dina ya nguvu kabisa ambayo niliipata nikiwa Katika Jiji la Mzuzu nchini Malawi ambapo waandishi wa habari wa Tanzania walikutana na wale wa Malawi na hali ya mazungumzo ilikuwa safi sana lakini hapa kubwa zaidi nakuletea jinsi nilivyofurahia dina yangu na kula kwa Mara ya kwanza kabisa nchini malawi . Ingawa wali ni ule ule,ugali ni ule ule halikadhalika mboga lakini mapishi ndio yalikuwa mapya sana. Hakika tembea uone ungana nami hapa

Hapa kulia kwangu anaitwa Chimwemwe huyu ni jamaa yangu ambaye pia alikuwa na idea ya hii misosi hapa mimi nilipenda nijipakulie tuu kimpango wangu .
Hapa ndio full misosi kujisevia kwa kwenda mbele hapa kulikuwa na Viazi vya kupondwa, wali mweupe lakini wa kichemsha, wali wa rangi sio biriani,kulikuwa na ugali lain si wa kisukuma lakini wa kawaida lainiii,pia kulikiwa na kachumbali,pilipili mahanjumati na munya munya za kutosha. Hakika haya yalikuwa ni mapishi mapya sana kwangu
Hapa nikiwa nateta jambo na jirani 
Hapa pia kulikuwa na kuku wa mchuzi kuku Bbq na kuku wa kuchemsha.. wote wa kienyeji. hii ilikuwa ni kumbukumbu tosha ya ukarimu wa watu wa Malawi.

Hizi ni safari na matukio

No comments: