Unaambiwa hivii tembea uone mengi. Kuna siku nilisha wahi kusema kuwa utalii sio lazima uende ukatazame wanyama ,ukaogelee ukatazame maeneo ya kihistoria lakini utalii wa kutembea pia ni muhimu sana.katika picha hii nilikuwa natoka zangu Jijini Mzuzu malawi kuelekea Lilongwe sasa nilipofika huko kati nikiwa nimeshikiria usukani kwa mbele niliona jamaa wamekamatia vitu mimi nikajua yes.. wanauza nyama hawa .. lakini nilipo karibia zaidi nikapunguza mwendo na kupaki pembeni. Jamaa kibao wakaja kunilaki na hawa ndege wanaitwa Njuni basi na mimi ikabidi niwaungishe.. kwa hakika walikuwa watamu sana. Hapa nikiwa nimewashika kuthibitisha kuwa ni kweli niliwaona .
Pichani ni mmoja ya madogo ambao wanauza ndege hawa. Lakini swali kuu hapa lilikuwa nu kwamba kuna idadi ya watu wengi wanauza ndege hawa. Je hakuna dalili ya wao kuja potea kabisa? maana hii ni lasilimali ingawa pia ni kitoweo.
Ukitazama dirishani utamuona mdau mwengine anao wauza ndege hawa. Kwa mujibu wao walisema hii ni biashara ya kawaida sana kwao
Hii ni katika Safari zangu za hapa na pale tunaungana na wadau wangu wa ukweli kwa njia hii hapa
No comments:
Post a Comment