NI Jumanne tena jamani! Wapenzi wasomaji wa safu yangu hii ya maisha na mapenzi tunakutana tena huku nikisema nawapenda sana.
Mada yetu ya leo ni kujisifu, wanawake hawapendi kusikia. Hii ni mada pana kidogo ambayo wanaume ni walengwa wakubwa lakini wenyewe hawajui.
KABLA YA MADA
Kabla ya mada nachukua nafasi hii kusema kuwa, mara zote ninapoandika jambo f’lani huwa nafanya uchunguzi wa kina kwanza kwa wahusika wachache ambapo hesabu za haraka huniambia ukweli unakuwa wapi!
TURUDIE MADA
Wiki iliyopita nilibahatika kuzungumza na wanawake kadhaa kuhusu tabia ya baadhi ya wanaume wanapokuwa kwenye jumuiya na wanawake wakiwemo, hupenda kujisifia kwa kujitangaza uwezo, mali, elimu na mambo mengine ambayo huamini wanawake wakisikia wanaweza kuwapenda wakiwatokea.
WALICHOSEMA WANAWAKE
Katika wanawake kumi niliozungumza nao, nane walionesha kukerwa na wanaume wenye tabia ya kujisifu mbele ya wanawake hata wanapokuwa na wanaume wenzao.
MMOJAMMOJA
Mama Simon wa Sinza B, Dar yeye alisema kuwa, kwake ameshakutana na wanaume wenye tabia hiyo na aliwatosa walipomtokea.
“Kuna mwanaume mmoja alikuwa akinitaka kimapenzi. Sasa kilichokuwa kikiniboa ni tabia yake ya kujisifu mbele za watu. Tukikaa mahali mfano na wenzangu na yeye akiwa na wenzake, ilikuwa lazima aseme ana uwezo mkubwa, anajenga Bunju, ana nyumba Kimara, anataka kuuza gari mara ameagiza lingine, hapendi kuvaa suti mpaka inapauka.
“Ile tabia ikawa inaniboa sana mimi kiasi kwamba ilibidi niwaambie wenzangu. Kumbe na wao walikuwa wakiboreka na ile tabia lakini walikuwa wakishindwa kuniambia.”
Mama Mudy, mkazi wa Mbezi Shamba (Mbezi ya Kimara), yeye alisema:
“Kusema ukweli, mimi mwanaume mwenye tabia ya kujisifu sipendi hata kumsikia. Sisi wanawake hatuhitaji sifa, tunataka mapenzi ya kweli na ya dhati. Ukijisifu kwa uwezo wako mimi nafaidika na nini?
“Mbaya zaidi wanaume wengi wanapenda kujisifia bila kujua wanawake hatupendi kabisa habari za majisifu. Wewe kama unampenda mwanamke mwaga sera siyo kujisifu.”
Siwezi kuandika maoni ya wanawake wote niliozungumza nao lakini karibu wote tena kwa nyakati tofauti walionesha kukerwa na tabia ya wanaume kujisifia mbele za watu.
Wengi walisema hawapendi kujua cheo cha mwanaume kazini, lakini wanashindwa kuelewa wanaume wenye tabia hii wanaulewa wa namna gani!
WANAUME NAO
Niliamua kuzungumza na wanaume wawili kuhusu hoja ya kujisifu, wote walisema wanawake wa siku hizi bila kuwaingia na ‘gia’ kubwa ni wagumu.
“Kujisifu muhimu kaka. Unajua wanawake ndiyo wanachangia, wanapenda sana kujua mwanaume ana nini? Mwanaume kama huna gari, mwanamke humpati. Anapenda mwanaume awe na gari, maisha mazuri nakadhalika,” alisema Ibrahimu, mkazi wa Kimara-Bunyokwa, Dar.
Hata mimi mwandishi wa mada hii nakubaliana na wanawake wenye kukerwa na tabia ya wanaume kujisifu mbele ya wanawake kwa kutangaza vyeo vyao au uwezo kuwa ndiyo gia ya kumpata mwanamke.

Kama unavyo unavyo tu, vitaonekana tena katika mazingira ambayo mwanamke atafurahi sana. Kama mwanamke hang’oki mpaka misifa, basi wenyewe wanasema hawatakiiii!!!
GPL
No comments:
Post a Comment