Mungu
ni mwema! Leo kama ada tunakutana mpenzi msomaji wangu wa Love &
Life katika kilinge chetu hiki kwa lengo la kuelimishana na kukumbushana
masuala ya mahusiano ambayo yametawala kwa kiasi kikubwa maisha yetu.
Tukubaliane kwamba, kutendwa au kuachwa kwenye mapenzi ni jambo la
kawaida. Watu wengi wamewahi kuachwa na wapenzi wao na katika hali
nyingine watu haohao waliotendwa huweza kuwaacha wapenzi wengine
waliowapenda; yote hii ni kawaida, lakini hali hii huwa tatizo pale
ambapo mtu anayeachwa au kuumizwa anakuwa ni yuleyule.
Mpenzi msomaji wangu, ni kweli kwamba tatizo hilo halijali mwonekano mzuri wa mtu au usiovutia, huweza kumtokea mtu yeyote na wakati wowote ule.
Mpenzi msomaji wangu, ni kweli kwamba tatizo hilo halijali mwonekano mzuri wa mtu au usiovutia, huweza kumtokea mtu yeyote na wakati wowote ule.
Swali la kujiuliza ni kwamba, kwa nini inatokea kwako kila mara? Nani
mwenye tatizo, wewe au wapenzi unaokutana nao? Ukiweza kujiuliza na
kupata ufumbuzi katika maswali hayo hakika utapata jawabu la jambo hili.
Tukumbuke kwamba, kuachwa au kutendwa muda mwingine huweza
kusababisha matatizo makubwa ikiwa muhusika amekabidhi asilimia kubwa ya
moyo wake kwa yule aliyenaye kwenye mahusiano.Mfano; mtu anaweza
kujiingiza kwenye masuala ya ulevi uliokithiri, utumwa wa mapenzi,
kujiua au kuua na matatizo mengine ya kisaikolojia.
Nikwambie tu kwamba, tatizo hili halihitaji mganga wa kienyeji
kulitatua, dokta au mchungaji kukuombea. Kikubwa unatakiwa kufahamu
mambo kadhaa ambayo kimantiki yanaweza kukusaidia ukadumisha uhusiano
wako na kuepukana na tatizo hili.
Fahamu, amekupendea nini?
Hili ni jambo kubwa na lenye maana kufahamu kama kweli unahitaji kudumu katika uhusiano wako. Suala hili halijalishi kuwa wewe ni mwanamke au mwanaume, ni wajibu wa wote kufahamu uliye naye anavutiwa na wewe kwa sababu gani.

Huenda
alikupenda kwa sababu wakati mnakutana ulikuwa ni mweusi unayeng’aa
lakini baadaye mkumbo wa ulimbukeni wa kuendana na wakati ukakupitia
hatimaye ukakuzoa kiasi cha kuanza kujibadilisha ngozi, maumbile na vitu
vingine.Kitu kidogo kwenye mahusiano kinaweza kusababisha madhara
makubwa sana!
Je, tabia zako zinaridhisha?
Usijifungie chumbani na kulia siku nzima au wiki huku ukihisi ukiwa mkuu kuwa wewe ni mtu mwenye mkosi usiye na thamani duniani.
Usijifungie chumbani na kulia siku nzima au wiki huku ukihisi ukiwa mkuu kuwa wewe ni mtu mwenye mkosi usiye na thamani duniani.
Ili kumaliza tatizo la kukimbiwa na wapenzi unao anzisha nao
mahusiano tumia muda mwingi kujipeleleza juu ya tabia ulizo nazo kuwa
zinaridhisha au la!Ikiwa ngumu kwako mwenyewe kugundua uzuri au ubaya wa
tabia zako, fanya upelelezi kwa kuwatumia marafiki na watu wako wa
karibu, inaweza kukusaidia pia kumaliza tatizo lako.
Wapo watu wanawakwaza wenzi wao kwa sababu ya kupenda kunung’unika
kupita kiasi, kusema uongo, ulevi na mambo mengine ambayo awali
hawakuwanayo.Mbaya zaidi wenzi wao wanapohoji kuhusu tabia hizo, huwa
wakali jambo ambalo siyo zuri.
Ukweli ni kwamba, sababu zipo nyingi sana za mtu kutodumu katika ndoa
au uhusiano anao anzisha, jambo la msingi si kutumia muda mwingi
kulaumu bali tumia muda mwingi kujiuliza unakosea wapi na rekebisha
makosa.
Tukutane wiki ijayo kwenye mada nyingine nzuri.
Tukutane wiki ijayo kwenye mada nyingine nzuri.
KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment